Jumatano, 12 Machi 2025

PROF. OLE GABRIEL :MAJENGO YA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI YAONESHA MATOKEO CHANYA

Na MAGRETH KINABO- Mahakama

 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel amesema Ujenzi Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (IJC) na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) umesaidia kuwawezesha wananchi kupata haki kwa wakati na kuwa wezesha kuendelea kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kuweza kukuza pato la Taifa na  uchumi wa nchi.

 

Aidha Prof. Gabriel amesema ujenzi huo na matumizi hayo akitolea mfano wa  ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji (IJC),Dodoma  ambao umesaidia kupunguza  mlundikano wa mashauri mahakamani  kwa  asilimia nne, ikiwa ndio lengo Mpango Mkakati wa  Mahakama ya Tanzania wa mwaka 2020/21-2024/25 na kuongeza kasi ya  uondoshaji wa mashauri kutoka asilimia  106, kikiwemo Kituo cha Utoaji Haki cha Masuala ya Familia(IJC), Temeke kichohudumia wastani wa wananchi 800 kwa siku.

 

Lakini Kituo hicho,kimefanikiwa kupunguza mlundikano wa mashauri kwa asilimia 1.4 kuongeza kasi ya  uondoshaji wa mashauri kutoka asilimia  106 hadi asilimia 91, ikiwemo kupunguza gharama za uendeshaji mashauri kwa Mahakama na za wananchi wanaofika mahakamani kwa ajili ya kupatiwa huduma za  haki kutokana na kuwepo huduma mbalimbali za Mahakama katika eneo moja.

 

Hayo yalisemwa na Mtendaji huyo wakati akiwasilisha taarifa ya mradi wa ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji(IJC),Dodomaleo tarehe 12 Machi, 2025 mara baada ya Wajumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) iliyoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Naghenjwa Kaboyoka kufanya ukaguzi kwenye jengo hilo.

 

“Dhana hii ya Kituo Jumuishi imebadilisha kabisa mtizamo wa Watanzania kwa huduma za Mahakama. Kabla ya kuwa na Kituo Jumuishi tulihudumia wateja kama 150 kwa siku kwa mtawanyiko. Lakini sasa ni zaidi ya wateja 500 kwa siku wanapata huduma za haki katika kituo hiki,” amesema Prof. Gabriel.

 

Amebanisha kuwa mashauri yanayosikilizwa katika Kituo hicho kuwa ni Ardhi,mauaji,talaka na ndoa,pia uwezo wa kutoa mashauri katika Kituo hicho ni siku 379 kwa mashauri ya madai na jinai siku 221 na Jaji mmoja anasikiliza wastani wa mashauri 294 kwa mwaka.

.

Ameongeza kwamba kuna watoa huduma wa msaada wa kisheria kutoka kwa wadau mbalimbali wa Mahakama ambao wako katika jengo hilo, wanawasaidia Watanzania hasa wa kipato cha chini kuweza kupata haki zao.

 

“Muda wa kutoa mashauri umepungua kutoka siku 730 katika kipindi cha mwaka 2020 hadi kufikia 380 kwa mwaka 2022. Hivyo   mabadiliko hayo yamebadilisha nidhamu ya Watanzania  huduma za Mahakama zinapatikana katika mazingira mazuri kama vile wako kwenye hoteli kubwa, ukilinganisha  na zamani, ambapo mahakama nyingi zilikuwa hali zisizoridhisha, amesisitiza.

 

Amefafanua kuwa baada ya miaka mitatu jengo kama hilo linahitaji kufanyiwa maboresho, hivyo suala la bajeti linatakiwa kuangaliwa kwa namna ya pekee.

 

 Prof. Gabriel ameishukuru Serikali kwa kutoa kipaumbele kwaujenzi wa  vituo hivyo sita  na sasa  vingine tisa  vinajengwa kwenye mikoa ya (Singida, Geita, Simiyu, Katavi, Njombe, Songea, Lindi, Songwe na Pemba sambamba na kunashukuru Bunge kwa ushirikiano na ushauri katika kupitisha bajeti ya Mahakama.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mhe. Kaboyoka  ame ya upongeza Uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa juhudi zao za kuhakikisha wananchi wanapata haki katika mazingira rafiki na kwa wakati.

 

Ujumbe huo ulitembelea  sehemu za mapokezi, Mahakama ya Watoto, ambapo walionesha kufurahishwa na madhari ya picha mbalimbali, ikiwemo Mahakama ya Wazi ili kujionea namna mashauri yanavyoendeshwa.

 

Baadhi ya wajumbe walitaka kufahamu Mahakama ina mpango gani wa kuhakikisha maeneo ya pembezo yanafikwa na huduma zake, akijibu swali hilo, Prof. Gabriel amesema kwa zipo Mahakama za Mwanzo 60 zinajengwa kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo maeneo hayo.

 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (Kulia), akiwaongoza viongozi wa Mahakama kuwapokea Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka(aliyevaa koti refu) kufanya ukaguzi kwenye jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji(IJC), Dodoma leo tarehe 12 Machi, 2025.

 


Baadhi ya Viongozi wa Mahakama ya Tanzania(kushoto) wakilisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka(aliyevaa koti refu).

 

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia), akitoa maelezo wa ujenzi wa mandhari ya nje ya jengo hilo kwa wajumbe hao.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) wakipata maelezo kuhusu chumba cha kunyonyoshea watoto kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia).

Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe. Anatropia Theonest akifurahia picha zilizopo kwenye Mahakama ya Watoto iliyopo katika jengo hilo huku akipiga picha.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) wakipata maelezo kuhusu sehemu ya chumba kinachotumiwa na Mahakama ya Watoto  kurekodi ushahidi wa mtoto kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(kushoto).

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) wakipata maelezo kuhusu  wananchi wanavyopata msaada wa huduma za sheria kupitia wadau wa Mahakama kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) wakipata maelezo kuhusu Mahakama ya Wazi  kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(aliyesimama).


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) wakipata maelezo kuhusu runiga inayotumika kuwaelimisha wananchi masuala ya haki na huduma za utoaji haki wakati wakisubiri muda wa kusikilizwa mashauri yao kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(aliyenyoosha mikono).

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa hiyo.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC)wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(hayupokatika picha).

Wajumbe kutoka  Hazina wakifuatilia taarifa hiyo.

 


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa hiyo. 


Mwenyekiti wa Kamati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) Mhe. Naghenjwa Kaboyoka akifualitia  kwa makini hoja za wajumbe. 
Mjumbe wa wa Kamati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) Mhe. Esther Matiko akiuliza swali.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel(aliyesimama) akijibu hoja za wajumbe wa Kamati hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni