Alhamisi, 13 Machi 2025

WANAWAKE MAHAKAMA KUU KANDA YA GEITA WALIVYOADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Wanawake wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita walishiriki kwenye Siku ya Wanawake Duniani ambayo iliadhimishwa tarehe 8 Machi, 2025. Walijadili kwa pamoja kuhusu Siku hii muhimu ambayo ni kumbukumbu ya ukombozi wa Mwanamke kwa kujadiliana masuala mbalimbali yalihusu Wanawake ikiwemo kufanya kazi kwa bidii, nidhamu, kuvunja ukimya dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa Wanawake, malezi mazuri ya familia ikiwemo watoto wao ili waweze kuja kuwa Wazazi na Watumishi wenye maadili mema katika jamii. Waliadhimisha siku hii kwa kufanya hafla fupi katika Hoteli ya Malaika Beach Resort iliyopo jijini Mwanza.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni