Jumamosi, 26 Aprili 2025

JAJI MAMBI AELEZEA ATHARI ZA KUTOLINDA TAARIFA BINAFSI

 Na INNOCENT KANSHA - Mahakama

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, Mhe. Dkt. Adam Mambi amesema kusipokuwa na msingi imara na mathubuti ya kiulinzi wa taarifa (Data Protection) kunaweza kuwa na madhira makubwa kwa mtu binafsi, hata kwa Taasisi, kiuchumi na ustawi wa jamii kiujumla katika Taifa.

Mhe. Dkt. Mambi aliyasema hayo alipokuwa anatoa mada kwenye Kongamano hilo inayosema Utatuzi wa Migogoro ya Kazi, Akili Unde na Ulinzi wa Taarifa katika mafunzo ya Usalama Mahala pa Kazi kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Taasisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja taasisi za kiserikali ambazo ni wadau wa mnyororo Mahakama Kazi.

Katika mafunzo hayo yalitolewa jijini Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa jengo la OSHA, na kubeba Kauli mbiu maalum kwa ajili ya kutafakari na kubadilishana uzoefu juu ya “Nafasi ya Akili Unde (Artificial Intelligence - AI) Mahali pa Kazi (Mapinduzi na Fursa)”

 Mhe. Dkt. Mambi amesema kukosekana kwa ulinzi wa taarifa kunaweza kuwa na madhara mbalimbali ikiwemo uvujaji wa taarifa na kupelekea taarifa nyeti kuvuja kama vile taarifa za watu binafsi, taarifa za kifedha hata kumbukumbu za nyaraka muhimu za kiusalama kwa Taasisi na Nchi kwa wadukuzi na watu wasiyo ruhusiwa kuzifikia taarifa hizo, matokeo yake inaweza kuwa, wizi wa mali au taarifa, ulaghai na pengine kupelekea usaliti.

Aidha, madhira mengine yanaweza kuwa ya kisheria, Mhe. Dkt. Mambi amesema, nchi nyingi duniani zimeweka mashariti, miongozo, sera na sheria kali za kulinda taarifa binafsi na pengine mtu anayekwenda kinyume na takwa hilo anaweza kuchukuliwa adhabu kali, kutozwa faini kubwa na kuburuzwa mahakamani ama kufungiwa maisha kufanya biashara kwa baadhi ya maeneo dunia.

Vilevile, Mhe. Dkt. Mambi ameongeza kuwa, kushindwa kulinda taarifa binafsi kunapoteza uaminifu kwa wateja na washabiki wa biashara husika ambayo mfanyabiashara ama Taasisi inayoendesha biashara ama mtoa huduma kwa kundi la watu fulani na kusababisha kupoteza mapato yaliyokuwa yanapatikana.

Amesema pia kuwa uaminifu ukivunjika ni vigumu tena kujenga taswira ya kampuni ama taasisi hiyo iliyokuwa ikitoa humuma husika kwa wateja au wananchi waliyokuwa wakiamini huduma husika.

Ametaadharisha madhara mengine ya kushindwa kulinda taarifa binafsi inaweza sababisha upotevu wa mapato kwa taasisi ama kampuni kutokana na fidia kubwa za kisheria ambazo zinagharimu fedha nyingi, ulaghai wa kutolinda mifumo ya taarifa binafsi na mifumo ya kibiashara ama kutoa huduma kuto aminika tena na wateja, hilo linapelekea wateja kugomea kutumia bidhaa za mtoa huduma hiyo na kusababisha aguko la kiuchumi kwa kampuni au taasisi husika na watu kupoteza kazi na stahiki husika.

Jaji Mambi ameongeza kuwa, kama taasisi itashindwa kulinda taarifa binafsi za wahusika wanaohudumiwa kunaweza kusababisha kupoteza imani na sifa ya taasisi iliyoijenga muda mrefu kulingana na shughuli za kutoa huduma fulani kwa wananchi. Hali hiyo inaweza kutangazwa katika vyombo vya habari kote na kupelekea washindani wa taasisi hiyo kutumia udhaifu huo kuididimiza taasisi hiyo katika kutoa huduma na kusababisha anguko la kiuchumi katika utoaji huduma kwa wananchi na kutoiamini tena na taswira yake kupotea kabisa katika ushindani wa utoaji wa huduma.

Mhe. Dkt. Mambi ameleza kuwa, kushindwa kulinda taarifa binafsi aidha kwa njia ya kupitia udukuzi unaosababishwa na kukua kwa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na mambo kama hayo kunaweza kusababisha anguko la uendeshaji wa taasisi katika shughuli zake za kila siku. Udukuzi huo unaweza kusababisha upotevu wa kumbukumbu za mafaili muhimu binafsi ya watu, mawasiliano binafsi na muhimu kwa njia ya imaili na hifadhidata kumbukumbu za wateja na hivyo kuathiri huduma zinazotolewa na taasisi.

Aidha Mhe. Dkt. Mambi ameongeza kuwa, kutolinda taarifa binafsi kunaweza kusababisha kupoteza ushindani wa kibiashara kwenye taasisi. Kushindwa kulinda taarifa za taasisi za kibiashara ama mipango ya uzalishaji wa bidhaa za kampuni kunaweza kuwasaidia washidani kuharibu shughuli za taasisi ama biashara taasisi inayofanya hivyo kuharibu uchumi na kuvurunga ustawi wa taasisi na wateja wake.

Ulinzi wa taarifa binafsi iwe kwa mtu binafsi ama taasisi ni muhimu ili kuokoa kupotea kwa mapato katika biashara, taarifa za watu akiwa hai ama amefariki ni lazima zilindwe kwa nguvu zote, taarifa binafsi zinamadhara kiuchumi na kijamii zinaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, Mhe. Dkt. Adam Mambi akifafanua mada ya ulinzi wa taarifa binafsi na athari zake kwenye kongamano la la mafunzo ya Usalama Mahala pa Kazi kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Taasisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja taasisi za kiserikali ambazo ni wadau wa mnyororo Mahakama Kazi.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, Mhe. Dkt. Adam Mambi akifafanua mada ya ulinzi wa taarifa binafsi na athari zake kwenye kongamano la  mafunzo ya Usalama Mahala pa Kazi kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Taasisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja taasisi za kiserikali ambazo ni wadau wa mnyororo Mahakama Kazi.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ya ulinzi wa taarifa binafsi na athari zake kwenye kongamano la mafunzo ya Usalama Mahala pa Kazi kati ya Mahakama Kuu ya Tanzania – Divisheni ya Kazi, Taasisi ya Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) pamoja taasisi za kiserikali ambazo ni wadau wa mnyororo Mahakama Kazi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni