Jumatatu, 28 Aprili 2025

LENGO LA MAFUNZO NI KUWATAYARISHA MSIFANYE MAKOSA WAKATI WA UTOAJI HAKI; JAJI MKUU

Na INNOCENT KANSHA-Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 28 Aprili, 2025 amefungua mafunzo elekezi kwa Majaji watano (5) wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania walioaminiwa na waliteuliwa kuwatumikia wananchi hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Majaji hao ni pamoja na Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Mhe. Latifa Mansoor, Mhe. George Masaju, Mhe. Dkt. Deo Nangela na Mhe. Prof. Agatho John Ubena.

Aidha Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo na ujuzi katika utoaji wa haki pamoja na kuwapatia muongozo na nyenzo muhimu ili kurahisisha utendaji wao wa kazi katika Mahakama ya Rufani.

Akitoa hutuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo yatakayo fanyika kwa muda wa siku tano yanayofanyika katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga Mhe. Prof. Juma amewakumbusha Majaji hao kuwa moja ya sababu ya kutoa mafunzo hayo ni kuwatayarisha kutofanya makosa juu ya dhamira ya dhati ya kutoa haki kwa wananchi pale wanapofika mbele yao.

“Akawakumbusha Majaji hao, kwa kutoa mfano wa maneno yaliyoandikwa na Lord Denning akasema, umuhimu wa uadilifu katika utoaji wa haki, hili ni jambo muhimu sana na haki inaanzia kwenye nafsi yako wewe yaani ndani, ukiwa na nafsi yenye kutenda haki siku zote utatafuta ukweli katika kila jambo unalolitolea maamuzi…

Na hapa ninapozungumzia haki, haki ni stahiki yako kwa mujibu wa Katiba na sheria huwezi kubakia ukisema nina haki nina haki, unaposema nina haki ni lazima ueleze chanzo chake na kiini chake ambayo ni Katiba au sheria, haki haipatikani tu hewani,” amesisitiza Jaji Mkuu Mhe. Prof. Juma.

Mhe. Prof. Juma amesema Jaji au Hakimu anayetoa haki lazima awe na dhamira ndani ya nafsi yake inayosimamia haki. Jaji Mkuu atolea mfano maneno ya Lord Denning kwamba, hakuna tija ya kuwa na sheria nzuri na unaweza kuwa na sheria nzuri kweli na zipo lakini sheria nzuri haitoshi kama mtekelezaji wa sheria hiyo hana kiini cha utoaji wa haki.

Aidha, Mhe. Prof. Juma ameongeza kuwa, maadili na utoaji haki siyo kwa Majaji na Mahakimu pekee hata kwa maafisa Mahakama wengine kama Mawakili uadilifu ni kwa wote, wengi huwa wanasahau kwamba sehemu kubwa ya haki inaanzia kwa Mawakili anapomshauri mteja, anaposimamia shughuli yake.

Wakili anapoanza kupoteza muda anamzungusha zungusha au anamwambia ukweli. Kwa mfano haki inaweza kupatikana kwa kufuata taratibu chache lakini wakili anaweza kuigeuza na kufanya biashara anaweza kupinda pinda maeneo mengi ilimradi apate kipato zaidi. Vilevile, wakili huyo anaweza kutoa hoja ambazo siyo hoja za kutenda haki, pengine hoja za kuwafurahisha wale wanaomlipa fedha na hilo ni jambo lililoandikwa na Lord Denning.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, haitakuwa na maana au tija hata kidogo kama tutakuwa na sheria sana kama zitasimamiwa na Majaji wabaya na wanasheria wasiokuwa waadilifu ama wala rushwa. Hicho ndicho kiini cha kazi ya utoaji haki kwa watu. Vilevile Jaji Mkuu Mhe. Prof. Juma akatoa rai na kuwakumbusha Majaji hao kutosahau kwamba wao wanatoa huduma za umma.

“Huduma za kimahakama ni huduma za umma kwa hiyo lazima tukubali kukosolewa sana kwa haki au hata kusikuwa kwa haki kwa sababu unafanya kazi ya umma na unapokosolewa usiichukulie kama suala binafsi, uchukulie kwamba ni sehemu ya kazi yako. Kuna wengine hawataki kuelewa ukweli, kuna wengine hawaelewi kweli na kuna wengine ambao hawataki ili shauri liishe wao linapoendelea ndiyo wanapata faida,” amesema Jaji Mkuu.

Mhe. Prof. Juma amesema, na mara nyingi maboresho yaliyo mengi yanatokana na kukusolewa, kwamba kuna maeneo ambayo yanalalamikiwa sana lazima watu wake na kuangalia kwa nini. Kwa mfano Mahakama ya Rufani imekuwa ikilalamikiwa sana kwamba maamuzi mengi yamekuwa yakiengemea sana mbinu au kanuni za kiufundi badala ya kuegemea kwenye haki. Jaji hawezi kukasilika anapokosolewa kwa hilo kwa sababu ni ukweli kinachotakiwa kufanyika kutafuta namna ya kukwepa kutumia kanuni za kiufundi.

Na kwa bahati nzuri sheria zimebadilishwa “overriding objectives” lakini baadhi yetu bado tunakwepa hata kutumia sheria hizi zilizobadilishwa bado tunaenda kwenye kanuni za kiufundi ambazo zinachukua muda mrefu sana katika utoaji wa haki.

Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul Faustine Kihwelo amewapongeza Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani wanaoshiriki mafunzo hayo kwa kuaminiwa na kuteuliwa na Mhe. Rais kuwatumikia wananchi.

Mafunzo haya ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya mafunzo ya Mahakama ya mwaka 2019, vilevile sera ya mafunzo ya Taifa ambayo inamtaka mtumishi yeyote anapoteuliwa katika nafasi mpya au kuajiriwa katika nafasi mpya anatakiwa kupata mafunzo elekezi na pia sera hiyo imesisitizwa katika Mpango Mkakati wa Mahakama na Mpango Mkakati wa Chuo.

“Mahakama ya Tanzania ni moja ya Taasisi chache sana ambazo zinafanya vizuri sana katika eneo la mafunzo kwa watumishi wa ngazi mbalimbali, hii ni kutokana na kweli kwamba tumekuwa kupokea maombi mengi kutoka taasisi mbalimbali zikitaka kuja kujifunza kupitia kwetu,” amesema Mkuu huyo wa Chuo.

Naye, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tanga Mhe. Katarina Revokati Mteule ameishukuru Mahakama ya Tanzania kuamuru mafunzo hayo kufanyika Kanda ya Tanga kwani Chuo cha Uongozi wa Mahakama kina Mamlaka pana kinaweza kufanya kazi mahali popote katika nchi lakini bado Kanda ya Tanga kupitia Chuo cha IJA kimepata heshima hiyo ya kipekee ya kuendesha mafunzo hayo elekezi kwa Majaji wa Rufani.

Akitoa ujumbe mfupi wa wananchi wa Kanda ya Tanga kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Mhe. Mteule amesema wanaTanga wanampongeza kwa maboresho makubwa yaliyofanya na Mahakama hasa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Aidha, siku ambayo waraka ulitolewa ukitaka kesi zote zisikilizwe kwa njia ya mtandao haraka sana Kanda ilichukua hatua kwa sababu jiografia ya Tanga ni ya kipekee kulinganisha na maeneo mengine ya nchi. Tanga ina wilaya nane na Mahakama za wilaya nane zote zipo mbali sana na inapopatikana Mahakama Kuu, amesema Mhe. Mteule

“Nikichulia mfano wa Wilaya ya Kilindi iliyopo zaidi ya kilometa 250 kutoka Tanga mjini ambapo wananchi wanasafiri umbali mrefu na miundombinu ya barabara siyo rafiki, hivyo kuanza matumizi ya kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao kumetoa fursa ya kuwapunguzia wananchi hawa gharama kubwa za uendeshaji wa kesi na kuokoa muda mwingi uliokuwa unapotea, sambamba na hilo imekuwa faraja kwao nakunitaka nikushuru sana kwa niaba yao Mhe. Jaji Mkuu,” amesema kwa bashasha Mhe. Jaji Mfawidhi huyo.

Majaji wanne kati ya hao watano, waliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mnamo tarehe 10 Januari, 2025 huku mmoja ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Feleshi aliteuliwa mnamo tarehe 14 Agosti, 2024. Wengine wanne ni Mhe. Latifa Mansoor, Mhe. George Masaju, Mhe. Dkt. Deo Nangela, na Mhe. Prof. Agatho John Ubena.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akifungua mafunzo elekezi kwa Majaji watano (5) wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania leo tarehe 28 Aprili, 2025 yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma  akifungua mafunzo elekezi kwa Majaji watano (5) wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania leo tarehe 28 Aprili, 2025 yanayofanyika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa mada ya wajibu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani katika msingi wa kukuza maboresho ya teknolojia mahakamani kwa Majaji Mahakama ya Rufani (hawapo pichani)

Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) Mhe. Dkt. Paul Faustine Kihwelo akifafanua namna Chuo hicho kinavyotekeleza Mpango Mkakati na sera ya Mafunzo kwa watumishi wa kada mbalimbali.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tanga Mhe. Katarina Revokati Mteule akitoa shukrani za wanaKanda ya Tanga kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma jitihada za kuboresha miundombinu hasa ya TEHAMA inavyosaidia wananchi kupata haki.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya akitoa neno la pongezi kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani kwa kuaminiwa na kuteuliwa kwao. 

Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. George Helbert akiongoza hafla hiyo ya uzinduzi wa mafunzo elekezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kutoka kwa mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof . Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)

Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kifuatilia hotuba hiyo kwa karibu

Sehemu ya Sekretariati ya mafunzo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kifuatilia hotuba hiyo.

Sehemu ya Viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa mafunzo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kifuatilia hotuba hiyo.
Sehemu Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kutoka kwa mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof . Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa mada ya wajibu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani katika msingi wa kukuza maboresho ya teknolojia mahakamani kwa Majaji Mahakama ya Rufani.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akitoa mada ya wajibu wa Majaji wa Mahakama ya Rufani katika msingi wa kukuza maboresho ya teknolojia mahakamani kwa Majaji Mahakama ya Rufani.

Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kutoka kwa mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof . Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)

Meza Mkuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani walioanza mafunzo elekezi Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.

Meza Mkuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Naibu wanasjili na Mahakimu mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo elekezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani alioanza leo Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.

Meza Mkuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo elekezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani yaliyoanza leo tarehe 28 Aprili, 2025 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.



Meza Mkuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma wakiwa kwenye picha ya pamoja na Sekretarieti ya mafunzo hayo mara baada ya hafla ya ufunguzi wa mafunzo elekezi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani yaliyoanza leo tarehe 28 Aprili, 2025 Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) mkoani Tanga.

Sehemu ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kifuatilia hotuba hiyo kwa karibu
Sehemu Majaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mafunzo elekezi kutoka kwa mgeni rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof . Ibrahim Hamis Juma (hayupo pichani)




Sehemu ya Viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa mafunzo ya Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kifuatilia hotuba hiyo.

(Picha na Innocent Kansha - Mahakama)





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni