Na NAOMI KITONKA- Mahakama, Dar es Salaam
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Mustapher
Mohamed Siyani jana tarehe 28
Aprili, 2025 aliongoza shauri
maalum kwa ajili ya kumuaga kitaaluma Jaji wa Mahakama hiyo, Mhe. Wilfred Peter Dyansobera, ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
Shauri hilo lilifanyika katika Ukumbi namba moja
(1) wa Mahakama Kuu jijini hapa na
kuhudhuriwa na Viongozi na Wadau mbalimbali wakiwemo Majaji wa Mahakama Kuu.
Akizungumza wakati wa kuendesha shauri hilo, oMhe.
Dkt. Siyani alisema kuwa jambo hilo ni muhimu kwa sababu linatoa nafasi kwa Mawakili wa
Serikali na Mawakili binafsi kuelezea jinsi wanavyowafahamu na kuwapima Majaji wanaostaafu kwa ajili ya
wengine kujifunza kupitia sifa zao.
“Mahakama
katika utendaji wake inathamini utendaji kazi wa Majaji
na kujituma kwao katika kukamilisha majukumu ya kimahakama
na hata pale wanapostaafu kwa mujibu wa sheria tunawapa nafasi Majaji na watoa haki wengine wajifunze
kupitia wengine pale sifa zao zinapotajwa na Wadau
mbalimbali wa Mahakama,”
alisema.
Akizungumza
katika moja ya mawasilisho yaliyotolewa, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanania, Kanda ya Dar es Salaam,
Mhe. Salma Maghimbi aliwakumbusha Majaji na Mahakimu kufanya wajibu wao kwa kufuata taratibu na sheria
zilizopo kwa mifano na kujifunza kwa vitendo ili kutimiza wajibu mkuu wa
Mahakama na kumaliza vizuri utumishi wao.
“Tunakupongeza
kwa kumaliza muda wako wa utumishi ukiwa na afya njema na katika kipindi chote utakumbukwa
kama mtafiti mzuri wa sheria, Mwalimu, mchapakazi, kaka, mwajibikaji na
tunaamini kwamba hautaenda kulala na badala yake utaendeleza ile ari ya
uchapakazi uliyoionyesha mahali hapa,” aliongeza Mhe. Maghimbi.
Alieleza kuwa wanatambua bidii kubwa
ya Mhe. Dyansobera katika kutetea na kutimiza majukumu ya kimahakama kwa kusimamia haki kwa Wananchi ikiwemo kutoa maamuzi ambayo
yanaendelea kusaidia kuamua kesi nyingine.
Akizungumza wakati wa shauri hilo, Mhe. Dyansobera
aliwashukuru wote kwa malezi mema, uongozi thabiti na mazingira bora ya kazi
yaliyochangia zoezi la upatikanaji haki kufanyika kwa urahisi, huku akisisitiza kuzingatia umuhimu wa
matokeo ya kazi na siyo muda mrefu mtu anaotumia kufanya kazi.
Naye Wakili wa Serikali, Bw. Camilius
Lugina alitoa pongezi na kwa upande wao akisema, “Mahakama imefanya jambo jema
na la heshima sana kwa kuwaaga Majaji wanaostaafu kwa sababu ni ishara ya
kutambua mchango wao mkubwa kwa Mahakama na namna taratibu za Mahakama
zinavyosaidia kurahisisha zoezi muhimu la utoaji haki ambalo ni jukumu kuu la
Mahakama.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Chama
cha Sheria Tanganyika (TLS), Wakili Ipilinga Panya alimpongeza Jaji Dyansobera
kwa kutenda kazi kwa uadilifu na weledi na
mchango wake ulioacha alama ya kudumu katika Tasnia ya Sheria Tanzania.
Zoezi
hilo la kuwaaga kitaaluma Majaji wastaafu linalofanyika kwa mujibu wa Walaka
Na. 1 wa Mwaka 2006 wa Jaji Mkuu na kuongozwa na Jaji Kiongozi lilihudhuriwa na Majaji wa Mahakama
Kuu, Wasajili wa Mahakama Kuu, Watendaji, baadhi ya watumishi wa Mahakama na Wadau mbalimbali.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilfred Peter Dyansobela (aliyeketi wa pili kutoka kulia waliokaa) pamoja na baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu walioshiriki katika shauri hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni