Alhamisi, 15 Mei 2025

JAJI MKUU AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU JAJI MANDIA KUTOA SALAAM ZA POLE

 SALAAM ZA POLE

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 15 Mei, 2025 majira ya alasiri amefika nyumbani kwa Marehemu Mhe. William Stephen Mandia, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania eneo la Oysterbay jijini Dar es salaam kutoa salaam za pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa na Marafiki kufuatia Kifo cha Jaji huyo Mstaafu kilichotokea tarehe 13 Mei, 2025 katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Jaji Mkuu Mhe. Prof. Juma alipowasili nyumbani kwa Marehemu alipata wasaa wa kusaini Kitabu cha maombolezo na kutoa salaam za pole kwa familia na wanajamii wa eneo hilo na kuwatia moyo kutokana na msiba huo na kuwaomba kuwa watulivu na kumuomba Mungu hasa katika kipindi cha majonzi ya kupotelewa na mpendwa wao.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiweka akisaini kwenye Kitabu cha Maombolezo alipowasili nyumbani kwa Marehemu Jaji Mandia Oysterbay jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Mei, 2025 alipofika kutoa salaam za pole kwa Familia ya wafiwa. 



Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa ameketi na Familia ya wafiwa pamoja na Viongozi waandamizi wa Mahakama mara baada ya kusaini Kitabu cha Maombolezo alipowasili nyumbani kwa Marehemu Jaji Mandia Oysterbay jijini Dar es Salaam leo tarehe 15 Mei, 2025 alipofika kutoa salaam za pole kwa Familia.






















Hakuna maoni:

Chapisha Maoni