Na Iman Mzumbwe – Mahakama, Songwe
Wafanyakazi wa Mkoa wa Songwe tarehe Mosi
Mei, 2025 walijumuika na wafanya kazi wengine katika maadhimisho ya siku ya
wafanyakazi Duniani ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Chama cha Mapinduzi
Vwawa Wilaya ya Mbozi.
Maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya
wafanyakazi kuanzia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mbozi na kuelekea katika uwanja wa
CCM Vwawa. Taasisi na Idara mbalimbali zilishiriki metembezi hayo na kupokelewa
na mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya Ileje Mhe. Farida Mgeni aliyemwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo.
Bi. Farida aliwapongeza wafanyakazi wote
kwa kufanya vizuri na kwa umoja wao aidha waliwapongeza wale wote waliofanikiwa
kuwa wafanyakazi hodari na alisema kuwa Tuzo walizopewa ziwe chachu ya kufanya
kazi vizuri na kwa bidii kwa kuzingatia kanuni, weledi na uaminifu. Serikali
ipo sukimamia haki za watumishi na wafanyakazi alisema Mkuu wa Wilaya huyo.
Aidha, Kwa upande wa Mahakama wafanyakazi
hodari waliopokea tuzo ni pamoja Mlinzi Mkuu wa Mahakama ya hakimu Mkazi Songwe
Bw. Sagala Simfukwe, Mlinzi wa Mahakama ya Wilaya Songwe Bw. Omary Osheni
Kihendu, Mlinzi Mahakama ya Wilaya Ileje Bw. Osward Enson Mwashitanda pamoja na
Msaidizi wa Kumbukumbu Mahakama ya Wilaya Momba Bw. Heny Japheti Mwakalinga.
Mgeni rasmi huyo katika hotuba yake
aliwahimiza wafanyakazi wote kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili kuleta
maendeleo ya nchi na amesisitiza waajiri watambue na kuwapa tuzo wanyakazi
hodari katika ofisi wanazosimamia. Vilevile alikemea tabia ya baadhi ya waajiri
kutoa zawadi hewa kwa wafanya kazi hodari na kuongeza kuwa hali hiyo inarudisha
nyuma morali ya kufanya kazi kwa wafanya kazi.
Siku ya wafanyakazi duniani kufanyika kila ifikapo tarehe mosi Mei ya kila mwaka Duniani kote ambapo wafanyakazi hupata fursa ya kuwasilisha changamoto zao kwa mwajiri ili ziweke kupata ufumbuzi ikiwa ni pamoja na suala la upandaji wa madaraja na ongezeko la mishahara.
watumishi
wa taasisi mbalimbali wakiwa katika matembezi kuelekea uwanja wa ccm Vwawa
ambako sherehe hizo zilifanyika.
wafanyakazi hodari wa Mahakama Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Bw. Sagala Simfukwe wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya sherehe hizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni