Jumatatu, 5 Mei 2025

WATUMISHI MAHAKAMA KANDA YA MOSHI WASHIRIKI MEI MOSI

Na CAREEN INOSHI- Mahakama, Moshi

Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda Moshi waliungana na Wafanyakazi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro kuadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani tarehe 1 Mei, 2025, ambayo kimkoa ilifanyika katika Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi.

Maadhimisho hayo yalianza na maandamano saa nne asubuhi kuanzia ofisi za TUCTA Mkoa wa Kilimanjaro na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Nurdin Babu, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

Wakati wa maadhimisho hayo kulikua na zoezi la ugawaji wa zawadi kwa Wafanyakazi bora. Watumishi wanne wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi ambao ni Wanachama wa TUGHE walipatiwa zawadi na mgeni rasmi ambazo ni vyeti pamoja na pesa taslimu.

Watumishi hao ni Bi.Lightness Mtey (Mahakama ya Wilaya Rombo), Bi. Junice Ngofi (Mahakama ya Wilaya Mwanga), Bw. Edward Mzava (Mahakama ya Wilaya Same) pamoja na Bi.Hajira Bundala (Mahakama Wilaya ya Hai).

Aidha, kwa upande wa Watumishi wa Mahakama ambao sio Wanachama wa TUGHE , Ofisi ya Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi iliandaa zawadi za ufanyakazi bora na hodari.

Watumishi hao ni Bw. Victor Zakaria (Mahakama Kuu Moshi), Bi. Regina Venace (Mahakama Kuu Moshi), Bi. Doreen Mwanri (Mahakama ya Hakimu Mkazi ), Bi. Esther Ikina (Mahakama ya Wilaya Moshi) pamoja na Bi. Sophia Kanje (Mahakama ya Wilaya Siha).

Sambamba na pongezi hizo, Watumishi pia walikumbushwa kujiunga na vyama vya Wafanyakazi kuendelea kufuata maadili ya kazi.


Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi wakiwa katika maandamano

 

 Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu ambaye alikua mgeni rasmi akitoa hotuba.

Mtumishi wa Mahakama ya Wilaya Rombo, Bi. Lightness Mtey akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora kutoka kwa mgeni rasmi.

Mtumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, Bw. Victor Zakaria akipokea zawadi ya Mfanyakazi bora kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Moshi Bi.Maria Itala.

 Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kusiriki maadhimisho hayo.

Habari hii imeghaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni