Na Daniel Sichula –
Mahakama, Mbeya
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga amesema
umoja na upendo ni nguzo muhimu katika kuwawezesha na kuwaweka watumishi pamoja, hayo yamejiri wakati akiwaongoza Waheshimiwa Majaji pamoja na Watumishi
waliozaliwa kuanzia mwezi Januari hadi Aprili, 2025
Aidha,
hafla hiyo ya kukata keki ililenga kuimarisha umoja na mshikimano kwa watumishi
pamoja na uongozi wa juu wa Mahakama Kuu Mbeya ulishuhudia viongozi na
watumishi waliozaliwa kuanzia mwezi Januari hadi Aprili, 2025 akiwemo Mhe.
Tiganga, Mhe. Said Kalunde pamoja na Naibu Msajili Mhe. Judith Lyimo pamoja na
baadhi ya Watumishi waliozaliwa tarehe na miezi tofauti tofauti Mahakamu Kuu
Mbeya.
Hafla
hiyo, iliyofanyika baada ya kumaliza kikao cha wiki cha watumishi na Uongozi wa
Mahakama kuu Mbeya. Viongozi wengine waliojumuika kwenye hafla ni pamoja na
Mhe. Jaji Victoria Nongwa, Mhe. Jaji Musa Pomo pamoja na Naibu Msajili Mfawidhi
Mhe. Aziza Temu.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda
ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (mwenye koti la Blue) akishirikiana na sehemu watumishi kukata keki wakati wa hafla hiyo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Said Kalunde (wa pili kulia) na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Judith Lyimo na sehemu ya watumishi wakikata keki katika hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (kushoto) akitoa shukrani kwa watumishi walioshiriki hafla hiyo.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akifurahia keki wakati wa hafla hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga (wa pili kulia) na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Said Kalunde (wa pili kushoto) na sehemu ya watumishi wakifurahia keki katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi wakifurahia keki katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi wakikata keki katika hafla hiyo.
Sehemu ya watumishi wakikata keki katika hafla hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni