- Akoshwa
na uboreshaji huduma za Mahakama unaoendelea kila uchwao
- Asisitiza
pia amani ya Nchi
Na MARY GWERA,
Mahakama-Dar es Salaam
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura ameipongeza
Mahakama ya Tanzania kwa kuendelea na uboreshaji wa huduma za utoaji haki
nchini.
Akizungumza leo tarehe 06
Julai, 2025 baada ya kutembelea Banda la Mahakama ya Tanzania lililopo kwenye
Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja
vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Temeke jijini Dar es Salaam, IGP Wambura
amekiri kufurahia hatua zaidi iliyopigwa na Mahakama nchini hususani katika
uboreshaji wa huduma zake.
“Nimefurahi sana
kutembelea banda hili la Mahakama, na mwaka jana nilikuwa hapa, mwaka juzi pia
nilikuwa hapa na sisi kama wateja wakuu wa Mahakama tumekuwa tukijifunza mambo
mengi hasa mapinduzi makubwa ya matumizi ya TEHAMA yanayofanywa na Mahakama
yetu ya Tanzania na mara kwa mara ninapokuja hapa kuna jambo ninajifunza na kwenda
kulifanyia kazi,” amesema Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi.
IGP Wambura amesema kuwa,
alipotembelea banda la Mahakama mwaka jana alijifunza juu ya matumizi makubwa
ya Ofisi ya Huduma kwa Mteja ya Mahakama na kukiri kuwa alivutiwa na eneo hilo
na kuwezesha pia kuanzia Ofisi kama hiyo katika Jeshi la Polisi.
Amesema kuwa, uanzishwaji
wa Ofisi ya Huduma kwa Mteja kwa Jeshi la Polisi umeleta mafanikio makubwa kwa
kuwa imewawezesha kupata mirejesho mbalimbali ikiwemo malalamiko kutoka kwa jamii
ambayo inawasaidia kuendelea kufanya uboreshaji wa huduma zinazotolewa na jeshi
hilo.
Aidha leo baada ya
kutembelea banda la Huduma kwa Mteja la Mahakama, IGP Wambura amepongeza
uboreshaji zaidi wa huduma zinazotolewa na Ofisi hiyo tofauti na ilivyokuwa
mwaka jana alipotembelea.
“Mwaka huu nimepita tena
Ofisi ya Huduma kwa Mteja (Call Centre) na nimekuta Mahakama imepiga hatua, sio
Call Centre ile niliyoiona mwaka jana na nasi tumejifunza ili tuweze kupiga
hatua zaidi kama wenzetu wa Mahakama kwakuwa katika Dunia hii watu hujifunza
kwa wenzao,” amesisitiza.
Kadhalika, Mkuu huyo wa
Polisi ameikaribisha Mahakama pia kutembelea Banda la Jeshi la Polisi ili nao
waweze kujifunza.
Kwa upande mwingine, IGP
Wambura amesisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kuilinda amani ambayo Tanzania
imebarikiwa nayo.
“Kwanza ni fahari kwa Tanzania kuwa na usalama kwa bara la Afrika na Duniani, hivyo niwahahakishie Watanzania kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia ipasavyo usalama na amani iliyopo, hivyo ni vema pia watanzania waendelea kuilinda amani iliyopo," amesisitiza Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi.
Viongozi mbalimbali wa
Mahakama na Serikali wameendelea kutembelea Banda la Mahakama ya Tanzania lililopo
kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea kufanyika hadi tarehe 13 Julai, 2025.
Banda la Mahakama ya
Tanzania linapatikana mkabala na Banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ndani ya
Viwanja vya (Sabasaba).

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akimsikiliza mtoa huduma kwenye banda la Mahakama la huduma kwa mteja Hakimu Mkazi Mhe. Adrian Richard Msisiri wakati alipotembelea katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara
ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akimsikiliza mtoa huduma kwenye banda la Mahakama la huduma kwa mteja Hakimu Mkazi Mhe. Adrian Richard Msisiri wakati alipotembelea katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akitoa maelekezo kwa maafisa wa jeshi hilo alipotembelea kwenye banda la Mahakama la huduma kwa mteja katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akisaini kitambu cha wangeni.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akipewa maelezo ya namna mifumo ya TEHAMA ya kimahakama inavyofanya kazi na Hakimu Mkazi Mkuu Mhe. Amani Peter Shao kutoka kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri (hayupo pichani).Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura (kushoto) akipewa maelezo ya namna shughuli za maboresho zilivyorahisisha utoaji haki mahakamani kutoka kwa Mtakwimu wa Mahakama ya Tanzania kutoka Idara ya Mipango Bw. John Magere na (hayupo pichani).
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura akifanya mahojiano na waandishi wa Habari alipotembelea Banda la Mahakama katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Temeke Dar es Salaam.

(PICHA NA INNOCENT KANSHA - Mahakama,Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni