Na ARAPHA RUSHEKE-Mahakama Kuu, Dodoma
Jaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju jana tarehe 4 Julai, 2025 alikutana na Majaji
na Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Dodoma na kufanya naye mazungumzo
mafupi.
Mazungumzao hayo
yalifanyika katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma na kuhudhuriwa na Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani na
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya.
Mhe. Masaju amewahi kuhudumu katika Mahakama hiyo kama Jaji wa Mahakama Kuu kabla ya kuteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt Mustapher Mohamed Siyani (aliyesimama)
akiwasalimia watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma.
Jaji Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju (kushoto) akipokea zawadi
kutoka kwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt
Julian Masabo.
Meza
kuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju
(aliyekaa katikati) kushoto kwake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani na kulia kwake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu
ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt Juliana Masabo ikiwa katika picha ya
pamoja na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma.
Meza kuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju (aliyekaa katikati) kushoto kwake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani na kulia kwake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt Juliana Masabo ikiwa katika picha ya pamoja na Naibu Wasajili pamoja na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania.
Meza kuu ikiongozwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju (aliyekaa katikati) kushoto kwake Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani na kulia kwake Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt Juliana Masabo ikiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Jaji Mkuu
wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju akikata keki aliyoandaliwa
na watumishi wa Mahakama Kuu Dodoma.
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama,Dodoma
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni