Alhamisi, 24 Julai 2025

TANZIA; DEREVA WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA, BW. MOHAMED MUSSA ZAHORO AFARIKI DUNIA


Marehemu Mohamed Mussa Zahoro enzi za uhai wake.

 TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Mohamed Mussa Zahoro aliyekuwa akifanya kazi Mahakama ya Rufani kama Dereva.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 24 Julai, 2025 na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Victor Kategere, marehemu Zahoro alifikwa na umauti jana Jumatano tarehe 23 Julai, 2025 Saa 4 Asubuhi katika Hospitali ya Royal mkoani Mwanza alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na changamoto ya Shinikizo la Damu.

Bw. Kategere amesema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika na marehemu Zahoro anatarajiwa kuzikwa Siku ya Ijumaa tarehe 25 Julai, 2025 Tanga Mjini. Marehemu Zahoro alizaliwa tarehe  14 Aprili, 1970.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu.

HAKIKA SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE YEYE TUTAREJEA (INNA LILLAH WA INNA ILLAH RAJIUN). 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni