Marehemu Sophia Bakari Mohamed enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake Bi. Sophia Bakari Mohamed aliyekuwa Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II katika Kituo cha Mahakama ya Rufani (T) jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo tarehe 19 Julai, 2025 na Mtendaji wa Mahakama ya Rufani (T),
Bw. Victor Kategere marehemu Sophia alifikwa na umauti Siku ya Ijumaa tarehe
18 Julai, 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma
alipokuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.
Bw. Kategere amesema
kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika na marehemu Sophia anatarajiwa
kuzikwa Siku ya Jumatatu tarehe 21 Julai, 2025 mchana katika Kijiji cha Nkinto Wilaya
ya Mkalama mkoani Singida. Safari kuelekea Kijijini Nkinto kwa ajili ya mazishi itakuwa tarehe 20 Julai, 2025 jioni baada ya ibada ya kumuaga marehemu nyumbani kwake Kikuyu mkoani Dodoma.
Marehemu Sophia alizaliwa tarehe 12 Aprili, 1996 na aliajiriwa na Mahakama ya
Tanzania tarehe 26 Julai, 2021 kwa Cheo cha Katibu Mahsusi (III) ambapo alipangiwa
Makao Makuu ya Mahakama sehemu ya Rasilimali Watu. Marehemu Sophia ameacha mtoto mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu kutokana na marekebisho ya Muundo yaliyofanyika mwaka 2023 marehemu Sophia alibadilishwa Cheo na kuwa Mwandishi Mwendesha Ofisi II.
Mwaka 2024, marehemu
Sophia alihamishiwa Kituo cha Kazi cha Mahakama ya Rufani alipohudumu kwa cheo hicho hadi
umauti wake.
Mahakama ya Tanzania
inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha kuomboleza
msiba huo mzito wa kuondokewa na Mpendwa wetu.
BWANA ALITOA NA BWANA
AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni