Jumamosi, 5 Julai 2025

UADILIFU NI NGUZO KUU YA MTUMISHI WA MAHAKAMA; JAJI TIGANGA

Na Daniel Sichula - Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga amewata watumishi wa Mahakama za Mwanzo wilayani Mbeya na Mkoa wa Mbeya kwa ujumla kufanya kazi kwa uadilifu na weledi ili kulinda hadhi ya Mahakama.

Mhe. Tiganga akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mahakama za Mwanzo Wilaya ya Mbeya Mjini kuanzia tarehe 03 na 04 Julai, 2025 ametembelea Mahakama ya Mwanzo Igoma, Uyole, Mwanjelwa Mbeya Mjini, Iyunga, Mbalizi, Santilya, Ilembo na Mahakama ya Watoto Mbeya (Juvenille Court) kukagua baadhi ya majengo ya Mahakama za Mwanzo yanayojengwa ikiwemo Mahakama ya Mwanzo Mbalizi.

Aidha, Katika ziara hiyo Mhe. Tiganga alipokea taarifa za utendaji kazi wa   Mahakama zote za Mwanzo wilayani Mbeya na baada ya kuzipokea alitoa nasaa kwa watumishi wote wa Mahakama kufanya kazi kwa uadilifu na kilinda hadhi ya Mahakama.

“Watumishi wenzangu ni vizuri kulinda hadhi ya Mahakama kwa kufanya kazi kwa uadilifu, kwani kitendo chochote utakachokifanya ambacho ni nje ya uadilifu kinaweza kuchafua taswira ya Mahakama na kuonekana wote hatufai kuhudumia wananchi” alisema Mhe. Tiganga

Vilevile, Mhe. Tiganga aliwapongeza Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kwa kuendesha kesi kwa kutumia simu na kuweza kumaliza mashauri kwa wakati kulingana na Mashauri yanayoletwa mahakamani na pia alitoa kongole za pekee watumishi wa Mahakama ya Watoto Mbeya. 

“Ni chukue nafasi hii ya kipekee kabisa kwa kazi nzuri mnazofanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusaidia kuboresha maisha ya watoto walio katika shule za watoto watukutu”

Aidha, Mhe. Tiganga alipokea changamoto mbalimbali katika taarifa zilizotolewa ikiwa ni pamaoja na ukosefu wa vyumba vya Mahabusu kwa Mahakama nyingi za Mwanzo ambayo inapeleka baadhi ya mahabsu kutoroka na hio inatoka na kutokuwepo kwa vituo vya Polisi jirani na Mahakama hizo.

Katika ziara hiyo Jaji Tiganga ameambatana na Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Emily Temu, Mtendaji wa Mahakama Kuu Mbeya Bi. Mavis Francis Miti, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya Mhe. Zawadi Laizer, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Tedy Mlimba pamoja na Mahakimu Mkazi wa Mahakama zote za Mwanzo Wilayani Mbeya, Afisa Utumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbeya Bi. Odilia Mapunda.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akikagua ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mbalizi Wilayani Mbeya mkoa wa Mbeya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akikagua ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mbalizi Wilayani Mbeya mkoa wa Mbeya.



Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akikagua ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mbalizi Wilayani Mbeya mkoa wa Mbeya.

Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo wilaya Mbeya Mhe. Abdul-Azizi Nchimbi akisoma taarifa mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga.


Mhe Joachim Tiganga akikagua mpaka wa kiwanja cha Mahakama ya Mwanzo Iyunga Wilayani Mbeya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akikagua ujenzi wa Mahakama ya Mwanzo Mbalizi
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga (kushoto) akisalimiana na mwenyeji wake wakati wa ziara hiyo
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Charles Tiganga akisaini kitabu cha wageni wakati wa ziara hiyo


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni