Na Daniel Sichula- Mahakama, Mbeya
Jaji
wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Ferdinand L. Wambali ameongoza kikao cha
tathimini (Post session) ya uendeshaji mashauri ya rufaa za Mahakama ya Rufani
jijini Mbeya na kutoa rai kwa mawakili kuzingatia kanuni za Rufaa wakati wa
usikilizaji wa mashauri ya Rufani.
Aidha,
kikao hicho akilijumuisha Jopo la lililoundwa na Majaji Watatu wa Mahakama ya
Rufani chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Wambali, huku Majaji wengine wa Mahakama
hiyo walikuwa ni Mhe. Gerson J. Mdemu pamoja na Mhe. Latifa A. Mansoor.
Akitoa
taarifa ya tathimini ya uendeshaji wa mashauri kwa jopo hilo Naibu Msajili wa
Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Omary H. Kingwele alisema mashauri hayo
yamesikilizwa kwa asilimia themanini na tano (85%) na mashauri 9 yanasubiri
uamuzi, huku mashauri 13 yameamuliwa na mashauri 4 ya Rufaa yamehairishwa.
Vilevile katika mashauri yaliyoamuliwa mashauri ya jinai ni 6 na mashauri ya
madai ni 7.
Akifafanua
kuhusu sababu zilizopelekea usikilizaji wa mashauri hayo ya Rufani kufanikiwa
kwa 85% Mhe. Kingwele alisema ni kutokana na waadawa wa rufani hizo kufika kwa
wakati kipindi cha usikilizaji wa mashauri, mawakili wa wadaawa walifika kwa
wakati kwa kipindi chote cha usikilizaji wa mashauri.
Katika
taarifa hiyo Naibu Msajili huyo alitoa mapendekezo kwa wadau waliohudhuria kikao
hicho kuwa mosi, Mawakili wanatakiwa kujiandaa vyema katika kuwaongoza wateja
wao kabla ya kuanza usikilizaji wa mashauri, Pia kuongeza umakini katika
uandaaji wa vitabu vya rufaa.
Wakati
huohuo wadau kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Mawakili wakijitegemea, Mawakili
wa Serikali, Ofisi ya Waendesha Mashtaka walitoa maoni yao pamoja na ushari kwa
Mahakama ya Rufani Tanzania.
“Naomba
Mhe. Jaji wa Mahakama Rufani hukumu ziwezi kutolewa kwa wakati ilikusaidia watu
kupata haki zao mapema” alisema mmoja wa washiriki.
Vilevile
kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wenyeji ambao ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga, Jaji wa Mahakama Kuu
ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Said Kalunde, Jaji wa Mahakama ya Tanzania
Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa, Jaji wa Mahakama ya Tanzania Kanda ya
Mbeya Mhe. Musa Pomo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza
Temu, Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Mbeya Mhe. Zawadi Laizer, Hakimu Mfawidhi wa Mkoa
wa Songwe Mhe. Francis Kisheni, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mkazi Mbeya
Mhe. Teddy Mlimba pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi. Mavis
Miti.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mwenyekiti wa Jopo Mhe. Ferdinand Wambali (katikati) akifungua kikao cha tathimini ya vikao vya Mahakama ya Rufani vilivyofanyika jijini Mbeya (Post session) Majaji wengine wa Mahakama hiyo walikuwa ni Mhe. Gerson J. Mdemu (kushoto) pamoja na Mhe. Latifa A. Mansoor (kulia).
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Bi. Mavis Miti sambamba na washiriki wengine katika kikao cha tathimini cha Mahakama ya Rufani Tanzania Kanda ya Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni