Na ARAPHA RUSHEKE - Mahakama Kuu Dodoma
Watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe hivi
karibuni walitembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania pamoja na Kituo Jumuishi
cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma, kujifunza mambo mbalimbali ya kimahakama.
Baada ya kuwasili katika jengo hilo,
watumishi hao walipata fursa ya kuonana na kufanya mazungumzo na Mtendaji
Mahakama Kuu Kanda, Bw Leonard Magacha.
Akizungumza na watumishi hao katika Makao
Makuu ya Mahakama yaliyopo Tambuka Reli Dodoma, Bw. Magacha aliwafahamisha miundombinu
ya Mahakama pamoja mambo mengine ambayo yanafanyika katika jengo hilo.
Ziara hiyo ililenga kujifunza kuhusu
utekelezaji wa majukumu ya kimahakama, mifumo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano-TEHAMA, maboresho mbalimbali ya huduma kwa wananchi pamoja na
kubadilishana uzoefu katika utendaji kazi wa kila siku.
Watumishi hao walitembelea ofisi
mbalimbali ikiwemo chumba cha kunyonyeshea watoto, ukumbi wa mikutano, chumba
cha Watoto cha kusubilia, chumba cha mifumo ya TEHAMA pamoja na kituo cha
huduma kwa mteja.
Baada ya ziara yao, watumishi hao
walionesha kufurahishwa na uboreshaji wa miundombinu ya Mahakama na kuipongeza
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Uongozi wa Mahakama ya
Tanzania kwa kufanikisha kazi hiyo pamoja na maboresho hayo.
Waliahidi kutumia maarifa waliyoyapata kuboresha huduma kwa wananchi wa Songwe kupitia Mahakama zao.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda, Bw. Leonard Magacha (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka Mahakama Mkoa wa Songwe walotembelea jengo la Makao Makuu ya Mahakama.
Watumishi kutoka Mahakama Mkoa wa Songwe wakiwa katika picha ya pamoja eneo la Makao Makuu ya Mahakama.
Msanifu wa Majengo wa Makao Makuu ya Mahakama, Bw.Wolfram Mremi akiwapa elimu mbalimbali kuhusu jengo la Makao Makuu watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe.
Baadhi ya watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe wakiwa katika moja ya chumba cha watoto kilichopo Makao Makuu ya Mahakama wakati wa ziara hiyo.
Watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe wakiwa katika chumba cha mifumo kilichopo Makao Makuu ya Mahakama wakisikiliza kwa makini jinsi mifumo inavyofanya kazi kutoka kwa Ofisa TEHAMA, Bw. Richard Matasha (hayuko pichani).
Msanifu wa Majengo wa Makao Makuu ya Mahakama, Bw. Wolfram Mremi akiwapa elimu mbalimbali kuhusu jengo la Makao Makuu watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe.
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda, Bw. Leonard Magacha (wasita kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka Mahakama Mkoa wa Songwe walipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) Dodoma.
Watumishi
wa Mahakama Mkoa wa Songwe wakisikiliza maelezo kuhusu Kituo Jumuishi
cha Utoaji Haki (IJC) kutoka kwa Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda, Bw. Leonard
Magacha (hayupo pichani).
Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda, Bw. Leonard Magacha akiwaelezea mambo mbalimbali
watumishi wa Mahakama Mkoa wa Songwe walipotembelea Kituo Jumuishi cha Utoaji
Haki Dodoma (IJC).
Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni