Na. Yusufu Ahmedi - IJA
Katika
kuimarisha utafiti wa kisheria na kuwezesha utoaji bora wa maamuzi ya
Kimahakama, Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kushirikiana na
Taasisi ya Laws.Africa, AfricaLII na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la
Ujerumani (GIZ) zimeendesha mafunzo ya wakufunzi (Training of the Trainers) ya utafiti
wa kisheria kwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Wasajili na Mahakimu
Wakazi.
Mafunzo
hayo yamefunguliwa na Mkuu wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani
Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo Agosti 04, 2025 na yanafanyika katika Hoteli ya Four
Points jijini Dar es Salaam.
Lengo
kuu ni kuboresha uwezo wa washiriki katika utafiti wa kisheria na kuwaandaa
kuwa wakufunzi kwa wenzao.
Katika
hotuba yake, Mhe. Dkt. Kihwelo amesema kuwa utafiti wa kisheria ni nyenzo
muhimu katika utoaji wa maamuzi ya Kimahakama nani nguzo katika utawala wa
sheria.
Pia
aliongeza kuwa maamuzi yanayotolewa ni muhimu yakajengwa katika utafiti wa kina,
na kwamba uamuzi mzuri ni ule uliyofanyiwa utafiti.
“Maamuzi
yetu lazima yajengwe juu ya utafiti wa kina, na usiobebwa na hisia za upendeleo.
Uamuzi uliofanyiwa utafiti mzuri na kuandikwa kwa weledi hujenga uaminifu kwa
umma, imani ni muhimu pia kwa Mahakama,” alisisitiza.
Pia alibainisha kuwa utafiti wa kisheria hauishii tu katika kutafuta kesi au sheria, bali unahusisha uchambuzi yakinifu wa vyanzo vya sheria na matumizi sahihi katika mazingira husika ili kutoa maamuzi yenye msingi thabiti.
Aidha alitoa shukrani zake za dhati kwa Taasisi ya Kimataifa ya Laws.Africa, AfricaLII kwa kushiriki kuandaa mafunzo pamoja na Shirika la Kimataifa la Ushirikiano la Ujerumani (GIZ) kwa ufadhili wa mafunzo hayo.
Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Biashara Mhe. Dkt. Mwajuma Kadilu ambaye pia ni mwezeshaji wa mafunzo hayo, pamoja na wawakilishi kutoka GIZ Tanzania akiwemo Bw. Muhamet Brahimi, Meneja Mradi wa Ukuzaji wa Utawala wa Sheria na Mahakama Barani Afrika (ProLA).
Mkuu
wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo
akihutubia katika mafunzo hayo.
Mkuu
wa Chuo ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo
(katikati) akiwa na Majaji wa Mahakama Kuu katika ya mafunzo ya wakufunzi
(Training of the Trainers) ya utafiti wa kisheria. Kushoto ni Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora Mhe. Dkt. Adam Mambi na kulia ni Bw. Muhamet Brahimi, Meneja Mradi wa Ukuzaji
wa Utawala wa Sheria na Mahakama Barani Afrika (ProLA).
Washiriki
wakiwa katika mafunzo hayo
Washiriki
wakiwa katika mafunzo hayo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni