Na Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya
Jaji
wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Barkel Sahel ahitimisha vikao vya
usikilizaji wa mashauri ya rufaani kwa mafanikio mashauri yaliyokuwa
yakiendeshwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
Akisoma
taarifa ya vikao hivyo Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe.
Charles Magesa alisema kwamba mashauri 24 ya rufaa kati ya 25 yaliyopangwa
kusikilizwa yalisikizwa na moja lilihairishwa kwa sababu zilizokua nje ya uwezo
wa Mahakama hiyo, katika mashauri 24 yaliyosikilizwa mashauri 22 yametolewa
maamuzi na mashauri 2 yanasubiri kutolewa maamuzi.
Mhe.
Magesa ameongeza kuwa mafanikio waliyofikiwa ni sawa na asilimia 96 ya mashauri
yote yaliyosikilizwa na asilimia 91 ni kwa mashauri 22 yaliyotolewa maamuzi.
Aidha,
katika taarifa hiyo iliyotolewa iliainisha changomoto zilizojitokeza katika
usikilizaji wa mashauri ya rufani kuwa ni pamoja sababu za rufaa kujirudia rudia
na zingine kuchelewa kuwasilishwa.
Kwa
upande wa Mashataka changamoto iliyojitokeza ni kushindwa kuleta mashahidi mahakamani
hasa kwenye mashauri ya ubakaji na ulawiti kama vile Askari Polisi na Madaktari.
“Watu
wa Mashtaka nawasisitiza kuwafikisha mashahidi mahakamani wakati wa usikilizaji
wa mashauri ya rufani ili haki iweze kutendeka.” alisema Mhe. Sahel
Mhe.
Sahel aliwashukuru wadaawa wote kwa kuweza kufika mahakamani kwa wakati na kwa
ushirikiano walioutoa mpaka kufikia mafanikio na malengo ya usikilizaji wa
mashauri kwa kiwango cha asilimia 96.
Wajumbe
waliohudhuria kikao waliwapongeza Majaji wa Rufani kwa kazi kubwa waliyoifanya
ya kusikiliza mashauri hayo yaliyokuwa yamepangwa kusikiliza katika Jopo hilo.
“Waheshimiwa
Majaji tunawapongeza sana kwa kazi mliyoifanya, tunaahidi changamoto zote
zilizojitokeza tutazifanyia kazi na kuahidi kutojirudia tena kwa vikao vijavyo,”
alisema mshiriki kutoka Ofisi ya Mashtaka.
Vilevile,
katika kakio hicho kilihudhuriwa na Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya
Mbeya Mhe. Joachim Tiganga, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria
Nongwa, Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Musa Pomo,
Wengine
walioshiriki kikao hicho ni Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mbeya Mhe. Aziza Temu, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi.Mavis Miti,
Mahakimu Mkoa wa Mbeya na Songwe, Mawakili wa Serikali na Wakujitegemea, Afisa
Magereza, Askari Polisi pamoja na wawikilishi kutoka ofisi ya Waendesha
Mashtaka wa Serikali.
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Barkel Sahel (katikati) akiendesha kikao cha tathmini ya uendeshaji mashauri ya Rufani kilichoketi Mahakama Kuu jijini Mbeya
Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Charles Magesa akitoa taarifa ya tathmini ya uendeshaji mashauri hayo.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki katika kikao hicho cha mashauri
yaliyokuwa yakiendeshwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa (kushoto), Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Musa Pomo (katikati) na Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu wakifuatilia kikao hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni