Na. Iman Mzumbwe – Mahakama, Songwe
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya,
Mhe. Joachim C. Tiganga alifanya ziara katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe,
ambapo ziara hiyo ilikuwa na lengo la kutoa semina juu ya matumizi ya mtandao
kwa wanachama wa TMJA katika shughuli za kimahakama pamoja na kutembelea mradi
wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki IJC -Songwe.
Aidha, katibu wa chama cha TMJA Mhe, Komba
E. Tagha alisoma taarifa fupi juu ya maendeleo ya chama hicho na aliongeza kwa
kusema chama kinajumla ya wanachama 26, ambapo ndani yake kuna wanaume 20 na
wanawake 6 na wote hao ni wanachama hai, Mhe, Tagha alitaja malengo makuu ya
chama hicho kuwa ni kutoa elimu kwa wanachama na jamii lakini pia kuanglia
maslahi ya Majaji na Mahakimu.
Akizungumza na wanachama hao wa TMJA
katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe, Mhe, Tiganga aliwakumbusha
kuwa malengo makuu ya Mahakama ni kuboresha uelewa wa kisheria, kuimarisha
maadili ya kazi na kuhakikisha huduma zinapatikana kwa wakati na usawa kwa
wananchi wote.
Aidha mafunzo ya mtandao yaliandaiwa na msaidizi
wa sheria wa Jaji kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Adriano Mtafya ambaye
aliwasisitiza na kuwaasa juu ya matumizi sahihi ya mitandao na kuwa taarifa
zote zitumwe kwenye barua pepe ili kuepusha matumizi ya karatasi. Afisa huyo pia
alitoa mafunzo kuhusu mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri (e-CMS)
Data hubi, mahakama mtandao, ambapo alisisitiza na kutoa rai kwa wanachama hao kuhahikikisha
wanaijua mifumo yote ya Mahakama ili kurahisisha namna ya utendaji kazi kwa
sababu mhimili huo kwa sasa upo kidigitali zaidi.
Mhe, Tiganga alitembelea pia mradi wa
ujenzi wa kituo jumuishi Min IJC Songwe na kukagua maendelea ya utekelezaji wa
mradi huo akizungumza mara baada ya kutembelea mradi huo Mhe. Tiganga alisema
amefurahishwa na maendeleo mazuri ya mradi kwa hatua waliyofikia ni nzuri
tofauti na mwaka uliopita, aidha alimsisitiza mkandarasi wa mradi huo kuongeza
juhudi zaidi ya ujenzi ili kufikia malengo mradi huo.
Katika ziara hiyo Jaji Mfawidhi
aliambatana na baadhi ya viongozi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya akiwemo Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Jaji Victoria Nongwa, Naibu Msajili Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Aziza Temu, Kaimu Mtendaji Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya
Bw. Alintula Watson Ngalile, Tedy Mlimba kutoka Mahakama ya Wilaya Mbeya, Ayubu
shellimo kutoka Mahakama ya Mwanzo Uyole, na Abdulaziz Nchimbi kutoka Mahakama
ya Mwanzo Mbalizi.
Mhe, Tiganga alipokelewa na Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbozi Mhe. Nemes L. Chami, Mtendaji wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Songwe Bw. Sostenes Mayoka na Mhe. Magreth Kannonyele Mwenyekiti
wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Songwe.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim C. Tiganga akisaini kitabu cha wageni alipofanya ziara ya kikazi Mahakama ya Mkoa Songwe
Muonekano wa mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha
Utoaji Haki IJC -Songwe.
Katibu wa chama cha TMJA Songwe Mhe, Komba
E. Tagha akisoma taarifa ya chama kwa Mhe, Jaji Mfawidhi
Jaji Mfwidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya
Mhe Joachim C. Tiganga akisalimiana na wanachama wa chama cha TMJA Songwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni