Na. Fredrick Mahava- Mahakama, Sumbawanga
Kituo
cha Huduma kwa Mteja cha Mahakama ya Tanzania kimefanya ziara ya kikazi Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Sumbawanga na kuhimiza watumishi Sumbawanga kuendelea
kutoa huduma bora kwa wananchi wanaofika mahakamani, ziara hiyo ilifanyika
tarehe 25 September, 2025 ikiwa na lengo la kupokea malalamiko, maoni, mapendekezo
kuhusu huduma za Mahakama.
Ziara
hiyo ilingozwa na Bw. Yahya Abadalah ambaye aliambana na Shifaa Liwali pamoja Amina
Mbaga ambapo walipata wasaa wa kutembelea gereza lililopo Sumbawanga na kupokea
malalamiko, maoni, mapendekezo na maulizo kuhusu huduma zinazotolewa na
Mahakama.
Aidha,
walipata wasaa wa kuongea na wateja waliokuja kupata huduma mahakamani siku
hiyo na kupokea malalamiko, maoni, mapendekezo na maulizo kuhusu huduma zinazotolewa
na Mahakama.
Vilevile,
Kituo hicho cha Huduma kwa Mteja waliweza kufanya kikao na watumishi wa
Mahakama Kanda ya Sumbawanga katika ukumbi uliopo Mahakama Kuu Sumbawanga kikao
kiliongozwa na Mhe. Deontina Kashaija ambapo waliweza kupokea malalamiko, maoni, mapendekezo na maulizo
kuhusu changamoto za kiutumishi na huduma zinazotolewa na Mahakama.
Naye,
Bw. Yahya Abadalah aliwaeleza watumishi baadhi ya kero, malalamiko waliyopokea
baada ya kutembelea gereza la Sumbawanga na kutoka kwa wateja waliowakuta mahakamani
hapo wakisubiria huduma na kuwataka watumishi kujitahidi kutoa huduma bora.
Bw.
Abadalah alitoa salamu za pongezi kwa watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga
kwani kero nyingi walizopokea katika mkoa huo zilikuwa siyo za kimahakama bali
ni changamoto zinazotokea kwenya mabaraza ya ardhi.
Kwa
upande wake, Bi. Shifaa Liwali aliwaeleza watumishi kuwa Kituo cha Huduma kwa
Mteja kimeanzisha utaratibu wa kupokea malalamiko, maoni na mapendekezo kupitia
mitandao ya simu na Whatsap chatbot kwa namba O752500400. Sambamba na hilo
kituo kimeanzisha utaratibu wa kupokea kero zinazohusu watumishi wa Mahakama
kupitia namba 07930110002 au Whatsap kwa namba 07930810002.
Aidha,
Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga Bi. Irene Mlangwa alikishukuru Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa
kufanya ziara hiyo ya kikazi Kanda ya Sumbawanga na kuwataka watumishi kuendelea
kutoa huduma bora kwa Wananchi ili kupunguza kero na malalamiko yanayojitokeza
Wakati
wa kikao hicho watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga walipata wasaa wa
kuuliza maswali, kutoa salamu za pongezi kwa kituo, malalamiko na mapendekezo.
Mhe.
Deontina Kashaija akiongoza kikao kati ya Watumishi na Kituo cha Huduma kwa
Mteja walipofanya ziara ya kikazi Kanda ya Sumbawanga.
Mhe.
David Mbembela akichangia hoja wakati wa kikao kati ya watumishi na Kituo cha
Huduma Kwa Mteja.
Kaimu
Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga Bi. Irene Mlangwa akizungumza wakati wa kikao.
Watumishi
wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga wakisikiliza kwa makini wakati wa kikao
Bi.
Shifaa Liwali kutoka Kituo cha Huduma kwa Mteja akizungumza wakati wa kikao na
Watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga.
Bw.
Yahya ABadalah kutoka Kituo cha Huduma kwa Mteja akizungumza wakati wa kikao na
Watumishi wa Mahakama Kanda ya Sumbawanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni