Na MWANDISHI WETU-Mahakama, Mafia
Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi amewataka Maofisa Wakaguzi
wa Mahakama za Hakimu Mkazi, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo
kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kutimiza lengo la Serikali la
kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Mhe. Maghimbi alitoa wito
huo wakati anafungua mafunzo ya ukaguzi wa Mahakama na utekelezaji wa hukumu
kwa maofisa wakaguzi katika Wilaya ya Mafia.
Akizungumza wakati wa
mafunzo hayo, Naibu Msajili, Mhe. Beda Nyaki aliwahimiza maofisa hao kufuata
mwenendo ya kazi zao pamoja na kufanyia kazi mafunzo walioyapata katika utoaji
wa huduma zilizo bora kwa wananchi.
Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mhe. Jakline Lugemalila, akizungumza kwa niaba ya waliopatiwa mafunzo hayo, alitoa pongezi kwa Viongozi walioandaa na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika kwa kutoa huduma bora.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kinondoni, Mhe. Jakline Lugemalila akizungumza wakati wa mafunzo hayo.








Hakuna maoni:
Chapisha Maoni