Alhamisi, 25 Septemba 2025

UGENI MZITO WA MAHAKAMA YA TANZANIA NCHINI GAMBIA

  • Jaji Mansoor, Siyani waongoza ujumbe watu 19 kushiriki mkutano wa kimataifa
  • Mahakama ya Tanzania yachomoza tena uwasilishaji mada.

Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, akifuatilia Mkutano kutoka mbali Dodoma

Jaji wa Mahakama ya Rufani, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mhe. Latifa Mansoor, pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustafa Mohamed Siyani, wapo nchini Gambia kuongoza ujumbe wa watu 19 wanaoshiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Chama cha Mahakimu na Majaji wa Jumuiya ya Madola unaofanyika jijini Banjul.

Mkutano huo wa 20 unaofanyika mwaka huu wa 2025, the 20th Commonwealth Magistrates’ and Judges Association (CMJA) 2025 Annual Meeting, ulianza tarehe 21 Septemba, 2025 na utamalizika terehe 26 Septemba, 2025. Mkutano huo umehudhuriwa na jumla ya nchi 43 za Jumuiya ya Madola.

Rais wa Gambia, Mhe. Adama Barrow, alifungua Mkutano huo na katika hotuba, pamoja na mambo mengine, aliwakaribisha wanachama wote na kuishukuru CMJA kwa kuamua kufanya mkutano huo mkubwa nchini kwake.

Alieleza pia namna nchi yake inavyotekeleza demokrasia, utawala wa sheria na kuheshimu haki za binadamu, na kwamba nchi yake inajitahidi kwa kadri inavyowezekana kuwezesha Mahakama nchini kwake kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake Jaji Mkuu wa Gambia, kwa niaba ya Mahakama na jamii ya wanasheria wa Gambia, aliwakaribisha wanachama wote wa CMJA na kuwashukuru pia kwa kauli mbiu ya mwaka 2025 inayoenda kwa jina la “Innovation in Judicial Practice: Embracing change for a Better Future.”

Alieleza kwamba kauli mbiu hiyo inayoendana na uhalisia wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, ambapo Mahakama duniani kote zinakumbana na changamoto ya maendeleo kwenye sekta hiyo, hivyo imekuja kwa wakati muafaka kwani inawezesha kupata uzoefu kutoka mataifa mbalimbali kuhusiana na chanagamoto zinazoibuka kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kijamii au kijiografia.

Alisema kuwa uzoefu wa pamoja na ugunduzi unaotokana na maenedeleo ya sayansi na teknolojia utakuwa nyenzo muhimu wa kuleta ufanisi katika Mahakama, uwezo wa wananchi kufikia vyombo vya haki, na umma kujenga imani kwa Mahakama na kuifanya iweze kwenda sambamba na maendeleo ya sayansi na teknolojia bila kuathiri miiko, tamaduni na maadili ya kimahakama.

Katika Mkutano huo, yupo pia Jaji kiongozi wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yohane Masara, ambaye ameonesha ushirikiano wa kikanda na Makamu wa Rais wa CMJA Kanda ya Kati na Kusini mwa Afrika,ambaye pia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta.

Wapo pia Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Adam Mambi, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha na Mhe. Sharmillah Sarwat. Uwakilishi huo umeshirikisha pia Viongozi Waandamizi, akiwemo Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Nkya na Rais wa JMAT, Mhe. Elimo Massawe.

Wengine ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Katibu wa Jaji Kiongozi, Mhe. Aidan Mwilapa, Mhe. Maria Mrio, Mhe. Kifungu Mrisho, Mhe. Teddy Mlimba, Mhe. Mary Kallomo, Mhe. Devotha Kasebele, Mhe. James Mniko, na Mhe. Fratern Temba.

Kadhalika, uwakilishi wa Mahakama kutoka Tanzania unajumuisha wajumbe wawili kutoka Chama cha Maofisa wa Mahkama Zanzibar (ZAJOA), Mhe. Mohamed Sheni na Mhe. Muumin Kombo, wote Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar.

Wajumbe hao walitumia fursa hii kubadilishana mawazo na wenzao kutoka mataifa mbalimbali, kuimarisha ujuzi, na kujadili mikakati ya kuboresha utoaji wa haki. Uwepo w mkutano huo unathibitisha umoja na mshikamano kati ya vyama hivi viwili, ukihamasisha ushirikiano wa kudumu kwa maslahi ya mfumo wa kisheria wa Tanzania.

Tofauti na hotuba mbalimbali za Viongozi, jumla ya mada 21 zitawasilishwa na kujadiliwa. Mada hizo ni; “Innovation in Judicial Practice: Embracing Change for a better Future”, “More efficiency or more stress: Modern Technology in the Court Room?” na “A comparison of sentencing guidelines-do they help in sentencing or fetter judicial discretion?”,

Nyingine ni “Artificial Intelligence- Can judges effectively monitor its ethical use in the courtroom? “Innovation in Commercial Courts Procedures”, “Progress on the Commonwealth Military Justice Transformation Project’’, “Innovation to Procedures in Small claims Courts”, “Is it no longer possible to make innovations in longstanding religious and customary courts?” na “Innovations in Election Petition Courts”.

Mada nyingine ni “Innovations in labour/Industrial Courts”, “Economic and Financial Crimes in the digital Era and making criminals pay”, “Innovation in family courts procedures", “a fireside chat”, “The Nauru Declaration on Judicial wellbeing”, “New guidelines for appointments to Apex Courts”, “Do disciplinary hearing for Judicial Officers pass the test of fairness?”.

Pia kuna mada zinazohusu, “Preparing for retirement”, “Innovations by diverting female and youths from custody and the wider impact on society”, “Social media and the judiciary-is it used to hold us in to account or to attack us with no right to reply?”, “Innovations in judicial procedures and cooperation in international courts”, na “What kind of protections do the judiciary really need?”.

Wakati wa Mkutano huo, Mahakama ya Tanzania imepata heshima ya Wataalam wawili, ambao wamebobea kwenye maeneo mbambali, Mhe. Dkt. Mhe. Dkt Adam Mambi mbaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mhe. Mary Kallomo, ambaye ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Morogoro, kuwasilisha mada.

Mhe. Dkt. Mambi ametoa mada ya Economic and Financial Crimes in the digital Era and making criminals pay, huku Mhe. Kallomo akiwasilisha mada inayohusu Social media and the judiciary-is it used to hold us in to account or to attack us with no right to reply.

Katika mada yake, Jaji Mambi alielezea namna uhalifu unavyofanywa kwa njia ya mtandao wakati huu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia. Alieleza namna ambavyo wahalifu wanavyotumia teknolojia kufanya uhalifu ili kuepuka nikono ya kisheria.

Alitoa mifano kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu kuonesha namna baadhi ya wahalifu walivyoweza kufanya uhalifu kwa njia ya mtandao na ilivyokuwa vigumu kuwapata, maana haikuwa rahisi kuweza kujua ni sehemu gani hasa mhalifu alikuwa wakati anafanya uhalifu.

Anaeleza kuwa mawasiliano ya mhalifu huyo huonesha mzunguko katika nchi tofauti tofati na mabara tofauti, japo baadaye huweza kupatikana. Hivyo, alizishauri Mahakama kuendelea kujiimarisha katika teknolojia ili kuweza kuendana na matakwa ya maendeleo ya sayansi na teknololojia ili kukabilia na uhalifu unatendeka kimtandao hasa katika zama hizi za sayansi na teknolojia.

Kwa upande wake, Mhe. Kalomo alielezea changamoto za matumuzi ya mitandao inavyoweza kuathiri imani ya wananchi kwa Mahakama. Ameeleza namna Mahakama ya Tanzania ilivyoweka mikakati ya  kujenga imani ya umma kupitia mageuzi ya kidijitali kwa kusajili na kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao, sera za uwazi, huduma kwa mteja na programe za kuelimisha jamii juu ya huduma za Mahakama. 

Pia alipendekeza sera za miongozo za matumizi ya kijamii zitengenezwe, vitengo vya kufuatilia na kujibu taarifa potofu, elimu kwa umma, mafunzo ya maadili ya kidijitali kwa watumishi wa Mahakama na mikakati ya kitaasisi kukabiliana na chamgamoto za kidijitali bila kuathiri uhuru  wa Mahakama na kujengeana hali ya  ustahimilivu wa kitaasisi na kukubali mabadiliko.

Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Mhe. Aisha Ally Sinda naye ni miongoni mwa watoa mada, yeye anatarajiwa kutoa mada katika eneo la “What kind of Protection do the Judiciary really need?” na kwakuwa hakuweza kufika kutokana na majukumu mbalimbali, atawasilisha mada yake kwa njia ya mtandao.  

Washiriki wa Mkutano huo kutoka Mahakama Jumuiya ya Madola katika picha ya pamoja.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, Mhe. Dkt. Adam Mambi akiwasilisha mada na kujibu maswali kwa ufasaha wakati wa mkutano huo.



Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Morogoro akiwasilisha mada kwenye Mkutano huo wa kimataifa. Jambo hili ni heshima kubwa kwa Mahakama ya Tanzania kwa kupata wawakilishi wawili kuwasilisha mada.

Ujumbe kutoka Mahakama ya Tanzania [juu na picha mbili chini ukifuatili kwa karibu kinachojiri wakati wa Mkutano huo.



Ujumbe kutoka Mahakama ya Tanzania kwenye picha ya pamoja [juu na chini].





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni