Na NAUMI SHEKILINDI, Mahakama-Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Annamringi Macha amefurahishwa na kuipongeza Mahakama ya Tanzania kufuatia ujenzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) na kwamba hatua hiyo imeonesha kujali na kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki mapema ipasavyo.
Mhe. Macha alitoa pongezi hizo hivi karibuni alipotembelea Mradi huo ili kujionea maendeleo yake na jitihada zinazofanywa na Mahakama ili kusogeza huduma bora kwa wananchi wa Mkoa huo.
“Kwakweli Mahakama mmepiga hatua kubwa sana na niwapongeze kwa mradi huu, hii itasaidia sana kupunguza gharama kubwa kwa wananchi, pia mradi ni wa kisasa hata ujenzi wake unavutia ubora unaonekana, nawashukuru na niwape pongezi kwa hatua hii nzuri,” alisema Mkuu wa Mkoa huyo.
Mhe. Macha ambaye aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo walipata fursa ya kuona na kuelezwa namna jengo litakavyokuwa linafanya kazi katika kutoa huduma baada ya kukamilika kwake.
Aidha Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Bw. Gasto Kanyairita alimtembeza Mhe. Macha kwenye vyumba na kumuelezea kazi ya kila chumba na ofisi zote zilizopo kwenye jengo hilo.
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe. Annamringi Macha (wa kwanza kushoto) na wengine wakisikiliza maelezo kutoka kwa Msanifu Majengo wa Mahakama, Bw. Deogratius wakati Mkuu wa Mkoa huyo alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC)-Simiyu.Katikati ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Bw. Gasto Kanyairita.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo Jumuishi wa Utoaji Haki (IJC) Simiyu. Wa pili kulia ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu, Mhe. Gasto Kanyairita pamoja baadhi ya watumishi wengine wa Mahakama na wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu na wafanyakazi wa Mradi wa ujenzi wa jengo hilo.
(Habari hii imehaririwa na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
2.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni