Ijumaa, 19 Septemba 2025

TANZIA; MTUMISHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFARIKI DUNIA

 TANZIA

Bi. Febronia John Mayala enzi ya uhai wake 

Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake Bi. Febronia John Mayala ambaye alikuwa Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la I kilichotokea mnamo tarehe 16 Agosti 2025 katika hospitali ya Kamanga Wilaya ya Nyamagana Mkoa wa Mwanza

Kwa mujibu wa Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Bw. Tutubi Mangazeni marehemu Bi. Febronia aliajiriwa mnamo tarehe 21 Septemba, 2015 katika kada ya Msaidizi wa Kumbukumbu II.

Baada ya kuajiriwa alipangiwa Kituo chake cha kwanza cha kazi cha ajira huko Mahakama ya Wilaya Sengerema na baada ya hapo akahamishiwa Mwanza IJC ambapo alipangiwa Mahakama ya Wilaya Ilemela na baadaye kuhamishiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi mpaka umauti ulipomfika

Ameajiriwa na elimu ya Stashahada ya utunzaji wa kumbukumbu (Diploma in Record Management) katika Chuo cha Utumishi wa Umma tawi la Tabora

Marehemu Bi. Febronia anatarajiwa kuzikwa Mwanza katika makaburi ya Buhongwa leo tarehe 19 Septemba, 2025.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni