Ijumaa, 19 Septemba 2025

TLS YAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA JAJI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA

Matukio katika picha wakati Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walipokutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiwa na sehemu ya Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akizungumza jambo na sehemu ya Viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) waliomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025.

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Boniface Mwabukusi (kulia) akizungumza jambo na Jaji Mkuu (hayupo katika picha) wakati viongozi wa Chama hicho walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 19 Septemba, 2025. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Bi. Mariam Othman.
Mazungumzo yakiendelea.


Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimkabidhi Majarida ya Mahakama ya Tanzania (HAKI Bulletin) Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Boniface Mwabukusi walipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 19 Septemba, 2025 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozu kutoka TLS walipomtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wa nne kushoto ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Bw. Boniface Mwabukusi, wa tatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TLS, Bi. Mariam Othman na Viongozi wengine wa Chama hicho.

(Picha na MARY GWERA, Mahakama)








Hakuna maoni:

Chapisha Maoni