Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 01 Oktoba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha elimu ya sheria nchini.
Matukio katika picha ya mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju na Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria Tanzania.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) akiwa katika mazungumzo na sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria waliomtembelea leo tarehe 01 Oktoba, 2025 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria waliomtembelea Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 01 Oktoba, 2025. Kulia ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sundi Fimbo.
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini wakifurahia jambo wakati wa mazungumzo kati yao na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania walipomtembelea leo tarehe 01 Oktoba, 2025 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mahakama na sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini waliomtembelea leo tarehe 01 Oktoba, 2025 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Wa tatu kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, wa kwanza kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sundi Fimbo, wa tatu kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Bi. Frida Mwera Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, wa pili kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Dkt. Erasmo Nyika ambaye ni Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wa kwanza kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo, Dkt. Lugaziya Mutabaazi Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na wa pili kushoto ni Mjumbe wa Baraza, Bi. Clara Mramba ambaye ni Mwakilishi kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).
(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni