Na. Hilary Lorry –
Mahakama, Lindi
Mahakama
Kuu Kanda ya Mtwara ikijumuisha na Mikoa ya Lindi na Mtwara, imefanya sherehe
ya kuwaaga watumishi waliostaafu utumishi wa umma kufikia October 2025,
Sherehe
hiyo iliyofanyika ndani ya Hoteli ya Sea View Beach Resort iliyoko wilayani
Lindi ikiwakutanisha viongozi mbalimbali wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara
akiwemo Jaji Mfawidhi Mhe.Edwin Kakolaki, Jaji Saidi Ding’ohi,Jaji Martha Mpaze
,Naibu Msajili Mhe. Seraphine Nsana, Hakimu Mkazi Mfawidhi Lindi Mhe. Consolata
Singano, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mtwara Mhe. Charles Mnzava ambaye pia ndiye
aliekuwa Mshereheshaji wa shughuli hiyo.
Jaji
Mfawidhi wa Kanda ya Mtwara Mhe. Edwin Kakolaki katika sherehe hiyo
aliwapongeza watumishi waliostaafu kwa utumishi wao uliotukuka katika kutoa
huduma kwa wananchi kwa kipindi chote walichotumikia muhimili wa Mahakama.
“Kuna
msemo unaosema “Life begins at forty” kwa maana Maisha yanaanza ukiwa na miaka
arobaini. Lakini hiyo inatuhusu sisi tulio kazini. Ila kwa nyinyi wastaafu
tunasema “Life begins at sixty” hivyo kwenu nyie Maisha ndo kwanza yameanza.” alisisitiza
Mhe. Jaji Kakolaki.
Kwa
nyakati tofauti Watendaji wa Mahakama Kuu Mtwara Bw. Yusuph Msawanga na
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.Quip Mbeyela waliwashukuru sana
watumishi waliostaafu kwa utumishi wenye nidhamu kwa kipindi chote cha utumishi
wao.
Aidha,
amewaomba watumishi waliopo kazini kudumisha nidhamu mahala pa kazi na kuchapa
kazi kwa bidii kwani ni moja kati ya misingi ya ufanisi kazini.
Wastaafu
walioagwa walishukuru uongozi wa Mahakama Kanda ya Mtwara ukiongozwa na Mhe. Jaji
Kakolaki kwa kuwaandalia sherehe hiyo ambayo hawakutarajia ingefana kwa kiasi
hicho.
Pongezi
nyingi zilielekezwa kwa Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe hiyo Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi. Mhe. Consolata Singano Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi.
Quip Mbeyela na kamati nzima ya maandalizi ya Sherehe hiyo.
Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na Watendaji wa Mahakama ya Lindi na Mtwara, Mahakimu Wafawidhi wa Wilaya zote, Mahakimu Mahakama za Mwanzo na Maafisa wengine wa Mahakama Kanda ya Mtwara.
Wastaafu wakiwa ukumbini tayari kwa kuagwa
Wabobezi katika zoezi la ufunguzi wa Shampeni
wakitekeleza jukumu hilo kwa umaridadi
mkubwa.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe. Edwini Kakolaki (wa pili kushoto) akiwa na, Jaji Saidi Ding’oi, wakiingia uwanjani kusakata rhumba.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe.
Edwini Kakolaki (wa pili kushoto) akitoa zawadi kwa mmoja wa wastaafu katika
sherehe hiyo
Wastaafu wakikata keki katika sherehe hiyo
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara Mhe.
Edwini Kakolaki akigonga glass na Wastaafu kutakiana afya njema.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara Mhe.
Edwini Kakolaki (wa tatu kulia) wakigonga glass kutakiana afya njema katika
sherehe hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya
kuwaaga wastaafu Kanda ya Mtwara Mhe. Consolata Singano (aliyesimama mbele)
akitoa taarifa fupi ya sherehe hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Lindi Mhe.
Subilaga Mwakalobo (kushoto) akiwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya
Lindi Mhe. Khalfan O. Khalfan wakifuatilia sherehe hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni