Jumatano, 8 Oktoba 2025

VIONGOZI WA DINI WAENDESHA MDAHALO KWENYE MAFUNZO YA MAHAKIMU WAKAZI WAPYA

  • Jaji Kihwelo akutana nao kuzungumza mawili, matatu

 Na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dodoma

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto [IJA], ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo, leo tarehe 8 Octoba, 2025 amekutana na Viongozi wa Dini na kufanya nao mazungumzo mafupi.

Viongozi hao wametoka katika Mkoa wa Dodoma wakiwakilisha Kanisa Katoliki, Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Kanisa la Wasabato pamoja na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania [KKKT].

Mhe. Dkt. Kihwelo aliwaeleza Viongozi hao lengo la kukutana nao, ikiwemo kufahamiana na pia kupata muhtasari kwa nini wamekuja mahakamani kwenye mafunzo ya Mahakimu Wakazi wapya zaidi ya 80.

Mahakimu Wakazi hao jana tarehe 7 Octoba, 2025 waliapishwa na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju, kushika wadhifa huo na kuhimizwa kuzingatia viapo walivyoapa wanapotekeleza majukumu yao.

Baada ya mazungumzo hayo mafupi, Viongozi wa Dini hao walielekea kwenye ukumbi wa mafunzo uliopo Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, ambayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na IJA.

Wakiwa kwenye ukumbi huo, Viongozi hao, kwa nyakati tofauti, waliendesha mjadala kabambe uliowashirikisha na kuwapitisha Mahakimu Wakazi hao kwenye masuala mbalimbali yanayohusu imani na dini kwa ujumla.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto [IJA], ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo [juu na picha mbili chini] akizungumza na Viongozi wa Dini alipokutana nao ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 8 Octoba, 2025.


Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Patricia Kisinda akichukua kumbukumbu muhimu wakati wa mazungumzo hayo.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto [IJA], ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Kihwelo [wa tatu kutoka kushoto] akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Dini hao baada ya mazungumzo mafupi.
Viongozi wa Dini wakiwa kwenye ukumbi wa mafunzo yaliyoandaliwa kwa Mahakimu Wakazi wapya baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju. 

Mkurugenzi wa Mafunzo kwenye Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Patricia Kisinda akiwakaribisha Viongozi wa Dini hao pamoja na Mahakimu Wakazi kwenye mafunzo hayo.
Padri Jobys Tharayil kutoka Kanisa Katoliki Dodoma alikuwa wa kwanza kuazisha mdahalo kwenye mafunzo ya Mahakimu Wakazi wapya.

Sehemu ya Mahakimu Wakazi wapya wanaoshiriki mafunzo hayo [juu na chini] wakifuatilia kilichokuwa kinajiri.


Sehemu nyingine ya Mahakimu Wakazi wapya [juu na chini] wanaoshiriki mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri.


Sehemu nyingine ya tatu ya Mahakimu Wakazi wapya [juu na chini] wanaoshiriki mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni