Na. INNOCENT KANSHA - Mahakama
Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 26 Novemba, 2025 jijini
Dodoma amekutana na kufungua Kikao cha ujumbe wa Benki ya duania uliokuja
nchini kwa ajiri ya kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mahakama ikiwemo
ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vinavyoendelea kujengwa katika mikoa
tisa nchini ikiwa ni awamu ya mwisho ya ukaguzi kuelekea hatua za ukingoni.
Vituo hivyo vinavyojengwa
katika mikoa mbalimbali nchini na ambavyo vipo katika hatua tofauti tofauti
kuanzia mkoa wa Lindi, Songea kwa asilimia 77, Njombe, Songwe, Katavi kwa
asilimia 85, Singida, Geita kwa asilimia 94, Simiyu kwa asilimia 95 na Pemba
ikiwa ni sehemu ya kudumisha Muungano.
“Uongozi wote wa Mahakama
unayofuraha kwa ushirikiano ambao unatolewa na Banki ya Dunia katika
kuhakikisha miradi ya maboresho inaendelea vizuri na mambo yote mazuri
yanayofanyika ni kutokana na ushirikiao wenu wa dhati wa hali na mali. Pia
nichukue fursa hii kuishukuru time ya Maboresho ya Mahakama kwa kufanya kazi
usiku na mchana kuhakikisha miradi ya maboresho ya ujenzi wa miundombinu inakamiliaka
ifikapo Desemba 31, 2025,” ameongeza Mtendaji Mkuu.
Prof. Ole Gabriel amekiri
kupokea ushirikiano wa asilimia 100 kutoka kwa Ujumbe huo na kusema Mahakama
imejizatiti kama ilivyoahidi mwezi wa Pili mwaka huu walipokutana na kujadili
kama kweli miradi yote itakamilika kwa wakati uliopangwa. Mahakama bado ipo
makini kuhakikisha kwamba inasimamia miradi hiyo hasa kipindi cha mwishoni mwa kukamilishwa
miradi yote iliyoanzishwa katika awamu ya pili ya ujenzi Mahakama haitalegalega
hata kidogo.
Aidha, Mahakama
itaendelea kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba mambo yote yanakamilika
kwa wakati uliopangwa, niwahakikishie Banki ya Dunia kwamba, natoa shukrani
zangu kwa Timu ya ndani inayotekeleza miradi hiyo ikiongozwa na Jaji wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha.
Kwa upande
wake, Kiongozi wa Msafara wa Benki ya Dunia Bi. Christine Owuor, amepongeza
kasi ya maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki nchini
kwani kwa sasa hatua ni zuri ukilinganisha na miezi sita ya nyumba hali haikuwa
nzuri sana.
“Tulikuwa
hapa nchini mwezi wa tisa, 2025 katika mwendeleo za ziara ukaguzi wa miradi ya
Banki ya Dunia inayotekelezwa na Mahakama hii ni ziara ya mwisho ya utekelezaji
wa ukaguzi wa miradi hii kabla haijafika mwisho mwezi Desemba 31, 2025,”
amesema Bi. Christine.
Aidha,
ameongeza kuwa, malengo ya mradi hajabadilika na kumekuwa na majadiliano mazuri
kati ya Banki hiyo na wataalum wa miradi ili kufanikisha matokeo chanya ya
mradi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza maelekezo yalifikiwa katika ziara
iliyopita.
“Ziara hii
inaweza kuwa ya kipekee kwa sababu tutahitaji kufikiria na kutafakari namna
bora tutakavyo hitimisha miradi kwa ufanisi, tunahitaji kupata ripoti nyingi za
uwajibikaji na utekelezaji wa miradi zilizokamilika ili tuweze kukamilisha
miradi kwa wakati ndani ya siku mbili ya ziara,” amesema Mkuu huyo wa Msafara.
Aidha, Bi.
Christine amesema kuna vitu ambavyo Mahakama ya Tanzania imeviendeleza na
kuvisimamia kikamilifu kwa kipindi cha miaka yote 9 kama Chumba cha Ufutailiaji
na Taarifa za Utendaji wa Mahakama (Judiciay Situation Room) ambayo ni mfano
ambayo watu wanatoka nje kuja kujifunza na inavofanya kazi, hii ikiwa baada ya
Mahakama kwenda kujifunza nchini Kazakhstan, kitu kingine kulizishwa kwa huduma
kwa mteja (court services satisfaction) imepanda kwa kiwango kikubwa.
Mfumo wa Usimamizi wa Mashauri ya Mahakama kwa
Elektroniki (Electronic Case Management System) hilo ndiyo eneo
lililoleta mapiduzi makubwa ya utendaji wa mahakama hasa kuchakata takwimu,
kusajili mashauri ni maeneo ya kupigiwa mfano na nchi zimekuja kujifunza namna
ya uendeshaji, IJA e- learning Platform, baklong
clearance hiyo ni maeneo ya mfano.
“Kuna maeneo
yanaendelea kufanya vizuri kwenye miradi inayoendelea ya ujenzi kama Pemba,
Geita, Simiyu pamoja na Katavi na maeneo mengine ambayo tulikuwa tunayatilia
shaka utekeleza wake wa miradi yanaendelea vizuri na yanaridhisha. Hatukuweza kutembelea maeneo yote safari hii
lakini kutokana na ripoti ya maendeleo ya miradi yuyopewa tumefurahishwa nayo,”
amesisitiza Bi. Christine.
Vilevile, Bi.
Christine ameongeza kuwa, Ujumbe unatambua kuwa fedha zote za mradi zimekishwa
kutolewa ili kukamilisha utekelezaji wa miradi kwa miezi hiyo iliyobakia kwa
maeneo ambayo bado, Ujumbe hautegemei kurudishwa kwa fedha yoyote katika
kutekeleza shughuli zilizobaki kama ununuzi wa magari kuhakikisha yanaletwa kwa
wakati.
“Tumekuja
kwenye ziara hii tukiwa na furaha kwa kuona kwamba Mahakama ndani ya kipindi
cha miezi sita Mahakama imefanya kazi kubwa kutoka pale tulipokuwa tukiomba
mkopo wa awamu ya pili kufikia hapa tulipo, tuna toa shukrani zetu kwa timu ya
Mahakama na timu ya Banki ya Dunia kwa kuhakikisha tunafanikisha kile
tulichokuwa tunakitarajia,” ameongeza Bi. Christine.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Banki ya Dunia pamoja SO-Owners wa mradi wa Maboresho ya Mahakama.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akielezea jambo wakati wa kufungua kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia leo tarehe 26 Novemba, 2025 IJC jijini Dodoma kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Benki ya Dunia Bi. Christine Owuor
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akimsikiliza Kiongozi wa Msafara wa Benki ya Dunia Bi. Christine Owuor akisema jambo wakati wa kufungua kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia leo tarehe 26 Novemba, 2025 IJC jijini Dodoma kulia ni Mtaalum kutoka Benki ya Dunia Bw. Benjamin Mtesigwa.
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia
Sehemu ya wajumbe waliohudhuria ufunguzi wa kikao cha ujumbe wa Banki ya Dunia
(Picha na INNOCENT KANSHA- Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni