Na. REHEMA AWET – Mahakama, Mwanza
Mwili wa marehemu Abriel Ezekiel Lazaro aliyekuwa
Dereva wa Mahakama ya Wilaya Bunda umeagwa katika hospital ya Bugando mkoani
Mwanza. Baada ya zoezi la kuaga mwili huo wa marehemu ulisafirishwa kuelekea mtaa
wa Nzasa Kata ya Chanika Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam kwa ajili ya
maziko.
Akizungumza kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania Kaimu
Jaji Mfawidhi Mhe. Kassim Robert alitoa pole kwa wafiwa, familia, ndugu, jamaa
na marafiki waliohudhuria katika zoezi la kuaga mwili wa marehemu Abriel.
Aidha, aliwakumbusha waombolezaji hususani watumishi
wa Mahakama kuwa “kifo cha mtumishi mwenzetu kiwe chachu ya kuchapa kazi kwa
bidii na uwadilifu huku tukimtanguliza Mungu mbele katika kutekeleza majukumu yetu
kwani hatujui siku wa saa,” alisema Jaji huyo.
Naye, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Bw.
Tutubi Mangazeni alieleza namna ambavyo Mahakama imeshiriki katika taratibu zote
za kushughulikia maziko ya mtumishi huyu ikiwemo kuaga mwili wa marehemu,
kuusafirisha na baadaye kuupumzisha kwenye nyumba yake ya milele huko jijini
Dar es Salaam tarehe 28 Novemba, 2025. Aliongeza kuwa, Mahakama Kanda ya Mwanza
na Musoma zimetuma wawakilishi katika maziko haya.
Katika zoezi la kuaga mwili wa marehemu liliongozwa na
Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Kassim Robert, Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Emmanuel
Ngigwana, Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe.
Godfrey Ntemi Isaya, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Crisencia
Kisongo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Butiama Mhe. Judith
Semkiwa, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Nyamagana Mhe. Ramla
Shehagilo, Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Bw. Tutubi Deo Mangazeni, Mtendaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Bw. Leonard Maufi, na watumishi wengine wa Mahakama
Kanda ya Mwanza na Musoma.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Godfrey Isaya akiaga
mwili wa marehemu Abriel Lazaro
Kaimu Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Kassim Robert (wa pili kulia), Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe.
Emmanuel Ngigwana (wa tatu kulia), Jaji
wa Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi Mhe. Godfrey Isaya (wa pili
kushoto), Naibu Msajili Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Crisencia Kisongo (wa kwanza kulia), Mtendaji
wa Mahakama Kuu
Kanda ya Mwanza Bw. Tutubi Deo Mangazeni (wa kwanza kushoto), na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma Bw. Leonard Maufi (wa tatu kushoto)
wakizungumza baada ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu kumalizika.




Hakuna maoni:
Chapisha Maoni