Jumanne, 25 Novemba 2025

WATUMISHI MAHAKAMA KUU MBEYA WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA RUAHA

Na. Daniel Sichula – Mahakama, Mbeya

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Joachim Tiganga aliwaongoza watumishi wa Mahakama Kuu Kanda hiyo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya wanyama pori ya Ruaha (RUAHA NATIONAL PARK) iliyopo mkoani Iringa.

Aidha, Mhe. Tiganga akielezea lengo la Safari hiyo kwa watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya alisema, “Watumishi wenzangu tukiwa hapa tunafurahia utendaji wetu wa kazi na kufikia malengo yetu kwa mwakan huu, kwa kushirikiana na uongozi chini ya Mtendaji wa Mahakama Kuu Mbeya tukaona inafaa kufanya jambo hili kwa kupongezana na kuweza kurudi na hali mpya kazini,” alisema Mhe. Tiganga.

Vilevile, Mhe. Tiganga aliongeza kuwa, hiyo ni fursa ya kukuza utalii wa ndani na kujifunza jinsi wanyama wanavyoishi na kuona mazingira yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kubadili mazingira ya watumishi kutumia muda mwingi maofisini kuwatumikia wananchi.

Katika safari hiyo ya kitalii Majaji wengine wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya walioungana na watumishi wa Mahakama Kuu hiyo ni pamoja na Mhe. Said Kalunde, Mhe.Victoria Nongwa, Naibu Msajili Mfawidhi Mhe. Aziza Temu pamoja na Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Bi Mervis Miti.

Picha na matukio mbalimbali ya watumishi wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa katika Hifadhi ya Wanyama Pori Ruaha.

Picha na matukio mbalimbali ya watumishi wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa katika Hifadhi ya Wanyama Pori Ruaha

Picha na matukio mbalimbali ya watumishi wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa katika Hifadhi ya Wanyama Pori Ruaha.

Picha na matukio mbalimbali ya watumishi wa Mahakama Kuu Mbeya wakiwa katika Hifadhi ya Wanyama Pori Ruaha.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Mbeya katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya. 

Watumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya wakifurahia jambo walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya wanyama pori ya Ruaha (RUAHA NATIONAL PARK) iliyopo mkoani Iringa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni