Na. Hilari Gadiye Herman – Mahakama, Lindi
Mtendaji wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela amekabidhiwa samani za Majengo
matatu ya Mahakama za Mwanzo za Ndomoni iliyopo Wilaya ya Nachingwea, Mahakama
ya Mwanzo ya Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi na Mahakama ya Mwanzo Mtandi
iliyopo Wilaya ya Kilwa zote zikipatikana katika Mkoa wa Lindi.
Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni
kati ya Bi. Mbeyela kwa niaba ya Mahakama na Bw. Edger Steven Kiogolo kutoka
kampuni ya Martisayi ambao ni watengenezaji wa samani hizo.
Akizungumza katika zoezi la makabidhiano hayo
Mtendaji Mbeyela aliipongeza kampuni ya Martisayi kwa kukabidhi samani
zilizotengenezwa katika umaridadi na viwango vya kuridhisha.
“Nimevutiwa na ubora na mwonekano wa samani
za Mahakama hizi tatu hakika zinavutia na pia zimeongeza thamani katika majengo
yetu’’ alisema mtendaji huyo.
Aidha, Bi. Mbeyela amewataka watumishi katika
Mahakama hizo kutunza kwa juhudi zao zote samani zilizokabidhiwa, majengo na
mazingira kwa ujumla ikiwa ni shukrani kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwajengea
majengo hayo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano alikazia suala la utunzaji
mzuri wa samani hizo ili zitumike kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
“Naomba kila mmoja atambue ni jinsi gani
Mahakama ya Tanzania imetuthamini na kutupendelea Mkoa wetu wa Lindi kwanza kwa
kupata miradi hii ya ujenzi na zaidi kutupatia samani zilizotengenezwa kwa nakshi na viwango
vya kuvutia hivyo ni wajibu wetu
kuvitunza na kuvilinda,” alisema Mhe.
Singano.
Naye, Bw. Edger Steven Kiogolo kutoka kampuni
ya Martisayi aliushukuru uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi kwa
ushirikiano mzuri waliouonyesha katika kipindi chote walichokuwa wakitekeleza
jukumu lao la utengenezaji wa Samani hizo na kuwaasa watumishi katika Mahakama
hizo kuzitunza samani hizo.
Vilevile, Bw. Kiogolo kutoka kampuni ya Martisayi alitumia fursa
hiyo ya makabidhiano kuelekeza na kutoa darasa kwa watumiaji wa samani hizo
hasa juu ya matumizi sahihi ya Makabati ya kisasa ya
kutunzia majalada (Compactor File cabinet) zoezi ambalo liliwaacha watumiaji
wakiwa na uelewa wa kutosha wa matumizi sahihi ya makabati hayo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu Hakimu
Mkazi Wafawidhi Mahakama ya Wilaya ya nachingwea Mhe. Neema Mhelela, Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe. Subilaga Mwakalobo, Hakimu
Mkazi Mfawidi Mahakama ya Mwanzo Mipingo Mhe.Bahati Mollel na Hakimu Mkazi
Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Mtandi Mhe.Siraji Daudi Mussa walishukuru uongozi
wa Mahakama ya Tanzania kwa juhudi kubwa za kuhakikisha mosi wanapata Majengo
hayo ya kisasa na pili kupatiwa samani zilitengenezwa katika ubora wa namna ile
huku wakiahidi kuvitunza kwa juhudi zao zote.
Katika zoezi hilo la makabidhiano Mtendaji wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela aliongozana na Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano na Afisa
Ugavi Msaidizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Mvita Ahmadi kwa ajili ya
kuhakiki na kuingiza samani hizo katika Daftari la mali za Mahakama.
Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Mbeyela (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya Samani za Mahakama hizo tatu.
Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa
umaridadi wa hali ya juu.
Muonekano wa nje wa jengo la Mahakama ya
Mwanzo Ndomoni.
Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo
wakiwa katika Picha ya pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi
Lindi Mhe.Consolata Peter Singano aliyesimama katikati,kushoto kwake ni Hakimu
Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe.Subilaga Mwakalobo na kulia ni
Mhe.Bahati Mollel Hakimu Mkazi Mfawidhi mahakama ya Mwanzo Mipingo.
Muonekano wa Makabati ya Kisasa (Compactor)
ikiwa ni miongoni mwa samani zilizokabidhiwa katika Mahakama hizo tatu.
Bw. Edger Steven Kiogolo (aliyeinama) kutoka kampuni ya Martisayi
akitoa elimu juu ya matumizi ya Makabati hayo ya kisasa (Compactor).
Kaimu Afisa Utumishi Mahakama ya Wilaya ya
Lindi Bw. Selemani Chikumba (kushoto) akiongea jambo na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo
Mipingo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya
Lindi Mhe.Subilaga Mwakalobo wa pili kushoto akiwa na watumishi wa Mahakama
yaMwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi.
Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa umaridadi wa hali ya juu.
Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa
umaridadi wa hali ya juu.
.jpg)

.jpg)

.jpg)
.jpg)






Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.
JibuFutaMwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com