Ijumaa, 21 Novemba 2025

MAHAKAMA YAKABIDHIWA SAMANI ZA MAHAKAMA YA MWANZO NDOMONI, MIPINGO NA MTANDI

Na.  Hilari Gadiye Herman – Mahakama, Lindi

Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela amekabidhiwa samani za Majengo matatu ya Mahakama za Mwanzo za Ndomoni iliyopo Wilaya ya Nachingwea, Mahakama ya Mwanzo ya Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi na Mahakama ya Mwanzo Mtandi iliyopo Wilaya ya Kilwa zote zikipatikana katika Mkoa wa Lindi.

Makabidhiano hayo yalifanyika hivi karibuni kati ya Bi. Mbeyela kwa niaba ya Mahakama na Bw. Edger Steven Kiogolo kutoka kampuni ya Martisayi ambao ni watengenezaji wa samani hizo.

Akizungumza katika zoezi la makabidhiano hayo Mtendaji Mbeyela aliipongeza kampuni ya Martisayi kwa kukabidhi samani zilizotengenezwa katika umaridadi na viwango vya kuridhisha.

“Nimevutiwa na ubora na mwonekano wa samani za Mahakama hizi tatu hakika zinavutia na pia zimeongeza thamani katika majengo yetu’’ alisema mtendaji huyo.

Aidha, Bi. Mbeyela amewataka watumishi katika Mahakama hizo kutunza kwa juhudi zao zote samani zilizokabidhiwa, majengo na mazingira kwa ujumla ikiwa ni shukrani kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwajengea majengo hayo.

Kwa upande wake Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano alikazia suala la utunzaji mzuri wa samani hizo ili zitumike kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

“Naomba kila mmoja atambue ni jinsi gani Mahakama ya Tanzania imetuthamini na kutupendelea Mkoa wetu wa Lindi kwanza kwa kupata miradi hii ya ujenzi na zaidi kutupatia  samani zilizotengenezwa kwa nakshi na viwango vya kuvutia  hivyo ni wajibu wetu kuvitunza na kuvilinda,”  alisema Mhe. Singano.

Naye, Bw. Edger Steven Kiogolo kutoka kampuni ya Martisayi aliushukuru uongozi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha katika kipindi chote walichokuwa wakitekeleza jukumu lao la utengenezaji wa Samani hizo na kuwaasa watumishi katika Mahakama hizo kuzitunza samani hizo.

Vilevile, Bw. Kiogolo  kutoka kampuni ya Martisayi alitumia fursa hiyo ya makabidhiano kuelekeza na kutoa darasa kwa watumiaji wa samani hizo hasa  juu ya  matumizi sahihi ya Makabati ya kisasa ya kutunzia majalada (Compactor File cabinet) zoezi ambalo liliwaacha watumiaji wakiwa na uelewa wa kutosha wa matumizi sahihi ya makabati hayo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Kaimu Hakimu Mkazi Wafawidhi Mahakama ya Wilaya ya nachingwea Mhe. Neema Mhelela, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe. Subilaga Mwakalobo, Hakimu Mkazi Mfawidi Mahakama ya Mwanzo Mipingo Mhe.Bahati Mollel na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Mtandi Mhe.Siraji Daudi Mussa walishukuru uongozi wa Mahakama ya Tanzania kwa juhudi kubwa za kuhakikisha mosi wanapata Majengo hayo ya kisasa na pili kupatiwa samani zilitengenezwa katika ubora wa namna ile huku wakiahidi kuvitunza kwa juhudi zao zote.

Katika zoezi hilo la makabidhiano Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Godfrey Mbeyela aliongozana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe. Consolata Peter Singano na Afisa Ugavi Msaidizi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Mvita Ahmadi kwa ajili ya kuhakiki na kuingiza samani hizo katika Daftari la mali za Mahakama.

Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bi. Quip Mbeyela (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya Samani za Mahakama hizo tatu.

Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa umaridadi wa hali ya juu.

Muonekano wa nje wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Ndomoni.

Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo wakiwa katika Picha ya pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Mhe.Consolata Peter Singano aliyesimama katikati,kushoto kwake ni Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe.Subilaga Mwakalobo na kulia ni Mhe.Bahati Mollel Hakimu Mkazi Mfawidhi mahakama ya Mwanzo Mipingo.


Muonekano wa Makabati ya Kisasa (Compactor) ikiwa ni miongoni mwa samani zilizokabidhiwa katika Mahakama hizo tatu.

Bw. Edger Steven Kiogolo (aliyeinama) kutoka kampuni ya Martisayi akitoa elimu juu ya matumizi ya Makabati hayo ya kisasa (Compactor).

Kaimu Afisa Utumishi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Bw. Selemani Chikumba (kushoto) akiongea jambo na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mipingo.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe.Subilaga Mwakalobo wa pili kushoto akiwa na watumishi wa Mahakama yaMwanzo Mipingo iliyopo Wilaya ya Lindi.

Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa umaridadi wa hali ya juu.


Muaonekano wa samani zilizonakshiwa kwa umaridadi wa hali ya juu.


Maoni 1 :

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

    dawnacuna314@gmail.com

    JibuFuta