Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju amefanya uapisho wa Hakimu Mkazi mmoja, Mhe. Clarence Josemary Mhoja na kumsisitiza juu ya uadilifu, utii wa Sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.
Hafla fupi ya uapisho ilifanyika tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Akizungumza mara baada ya uapisho huo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Abdi Kagomba alimsisitiza Hakimu Mkazi huyo aliyeapishwa juu ya kumshirikisha Mungu katika kila jambo, kuwa muadilifu katika utendaji.
Kadhalika Mhe. Kagomba ameongeza kwa kumsisitiza Mhe. Mhoja kufanya kazi kwa weledi, kudumisha ushirikiano wakati wa kazi, kujiendeleza kielimu, kuwa mzalendo, pamoja na kuhakikisha kuwa taarifa za kiofisi hazitoki nje ya ofisi bila maelekezo maalum.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe.
George Masaju (kulia) akimuapisha Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Clarence Mhoja tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini
Dodoma. Anayeshuhudia katikati ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya.
Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Clarence Mhoja akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (hayupo katika picha). Hafla ya uapisho ilifanyika tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akisaini hati ya kiapo mara baada ya kumuapisha Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Clarence Mhoja (hayupo katika picha) tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania -Masjala Kuu, Mhe. Abdi Kagomba akizungumza jambo mara baada ya uapisho wa Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Clarence Mhoja (hayupo katika picha) tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi mpya, Mhe. Clarence Mhoja (kulia). Kushoto ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Abdi Kagomba mara baada ya uapisho uliofanyika tarehe 24 Desemba, 2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.
(Picha na JEREMIA LUBANGO, Mahakama-Dodoma)






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni