Jumatano, 21 Januari 2026

JAJI MKUU AFANYA MAZUNGUMZO NA BODI YA UDHAMINI WA TAARIFA ZA JUZUU LA SHERIA

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 21 Januari, 2026   ametembelea na kufanya mazungumzo na Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) inayoendelea na kikao kazi chake kwenye ukumbi wa Maktaba Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma.

Kikao kazi hicho ambacho kilianza tarehe 19 Januari, 2026 kinalenga kuchambua maamuzi ya mwaka 2025 ya Mahakama ya Rufani, Mahakama Kuu ya  Tanzania na Mahkama Kuu ya Zanzibar kwa ajili ya kitabu cha Mwaka 2025.

Kikao kazi hicho kinatarajiwa kuhitimishwa tarehe 23 Januari, 2026.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju akisaini kitabu cha wageni leo tarehe 21 Januari, 2026 alipoitembelea Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR)  na kufanya mazungumzo na Bodi hiyo inayoendelea na kikao kazi chake kwenye Maktaba ya Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma.

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Maktaba ya Mahakama katika kikao kazi cha Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) kinachoendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Maktaba ya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma. Aliyeketi mbele ni Katibu wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania Prof. Hamudi Majamba.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi katikati) akisikiliza kwa makini na kunukuu hoja za wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) wakati alipotembelea na kufanya kikao na Bodi hiyo leo tarehe 21 Januari, 2026 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma. Kushoto ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR), Mhe. Jacobs Mwambegele na kulia ni Katibu wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania Prof. Hamudi Majamba.


Sehemu ya wajumbe wa Bodi wanaohudhuria kikao kazi cha Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) kinachoendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma.

Sehemu nyingine ya wajumbe wa Bodi  ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) wanaohudhuria kikao kazi kinachoendelea kufanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani (wa kwanza kulia) wakisalimiana na wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) mara baada ya mazungumzo na wajumbe hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. George Masaju (wa tano kulia)  akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria Tanzania (TLR) mara baada ya mazungumzo na wajumbe hao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Maktaba uliopo Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma. Wa sita kulia ni Mhe. Jacobs Mwambegele, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Taarifa za Juzuu la Sheria  Tanzania (TLR) na wa kwanza kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.Dkt. Mustapher Mohamed Siyani.

(Picha na HABIBA MBARUKU, Mahakama-Dodoma)

 

 

 

 

 


 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni