Jumatano, 14 Januari 2026

JAJI MKUU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA INDIA NCHINI TANZANIA

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju leo tarehe 14 Januari, 2026 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Viongozi hao wamejadiliana kuhusu mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na ushirikiano kwenye masuala ya kisheria kati ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya India.

Yafuatayo ni matukio katika picha ya mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey na ujumbe alioambatana nao.



Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey alipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 14 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Mazungumzo yakiendelea...


Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Balozi wa India nchini Tanzania yaliyofanyika leo tarehe 14 Januari, 2026.


Katibu Binafsi wa Jaji Mkuu ambaye pia ni Naibu Msajili wa Mahakama, Mhe. Venance Mlingi akichangia jambo wakati wa mazungumzo kati ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Balozi wa India nchini Tanzania yaliyofanyika leo tarehe 14 Januari, 2026.

Ujumbe kutoka Ubalozi wa India wakiwa katika mazungumzo na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (aliyeketi mbele) leo tarehe 14 Januari, 2026 wakati Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey alipomtembelea Jaji Mkuu ofisini kwake jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akimpatia Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey nakala za Jarida la Mahakama ya Tanzania (HAKI Bulletin) wakati Balozi huyo alipomtembelea Jaji Mkuu leo tarehe 14 Januari, 2026 ofisini kwake Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey (kushoto) akimpatia zawadi Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju alipomtembelea ofisini kwake leo tarehe 14 Januari, 2026 Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Bishwadip Dey (wa tatu kushoto), Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (wa tatu kulia), Katibu Binafsi wa Jaji Mkuu ambaye pia ni Naibu Msajili wa Mahakama, Mhe. Venance Mlingi (wa kwanza kulia) pamoja Maafisa walioambatana na Balozi wa India.

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. George Masaju (kulia) akiagana na Balozi wa India nchini Tanzania mara baada ya kufanya mazungumzo leo tarehe 14 Januari, 2026 ofisini kwa Jaji Mkuu Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.


(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma)







 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni