Mhe. Jaji Crescencia
Makuru, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, akifungua rasmi mafunzo maalumu ya Huduma
kwa Wateja kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania, mkoani Dodoma.
Mafunzo
maalumu ya siku mbili yahusuyo huduma kwa wateja na haki ya kupata taarifa kwa
watumishi wa Mahakama, yameanza katika hotel ya St.Gaspar mjini Dodoma.
Akifungua
rasmi mafunzo hayo, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Crescencia Makuru,
amesema moja ya malengo makuu ya mafunzo hayo, ni kuwajengea uwezo watumishi wa
Mahakama kwa kuwapa mbinu na mikakati mbalimbali itakayowasaidia kuongeza
ufanisi katika utendaji kazi.
“Mahakama ya Tanzania kwa
sasa inaendelea na maboresho ya utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha
kuwa inatoa huduma iliyo bora na kwa wakati”, Jaji Makuru amebainisha.
Mwaka
2014 Mahakama ya Tanzania kama moja ya Taasisi ya Serikali ilifanyiwa tathmini
kuhusu utoaji wa haduma zake hasa katika nyanja ya upatikani na utoaji wa taarifa
kwa Umma iliyoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika,
(Media Institute of Southern Africa-MISA). Katika tathmini ile, Mahakama
ilikuwa ya mwisho na ilizawadiwa kufuli la dhahabu kama alama ya kuonyesha kuwa
taasisi hii ni moja kati ya zilizojifunga sana kutoa taarifa kwa wananchi. Moja
ya maeneo yaliyoonekana na udhaifu ni namna masijala za Mahakama zinavyopokea
na kutunza nyaraka na hata wanavyowahudumia wateja kwa ujumla.
Mafunzo hayo yamelenga
kuwafundisha makarani na watumishi wa kada mbalimbali nini maana ya uhuru wa
Habari na habari ni Nini?, Huduma kwa wateja na ujuzi wa mawasiliano kwa
watumishi wa Umma , Njia mbalimbali za upatikanaji wa taarifa katika Taasisi za
Umma na Sheria ya utoaji wa habari
katika Mahakama.
Mafunzo
haya yameandaliwa na kufadhiliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) pamoja na Taasisi ya
Friedrick Ebert Stiftung (FES) ofisi ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni