Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akikaribishwa
na viongozi wa Magereza Mkoa wa Ruvuma katika Ofisi za Magereza Mkoa wa Ruvuma.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania (aliyeketi) akisikiliza taarifa fupi kuhusu hali ya magereza kutoka kwa Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Ruvuma ACP Ally A. Kaherewa.
Mhe. John S. Mgetta Jaji Mfawidhi kanda ya Songea
(kulia), Mhe. Katarina Revocatti, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania (kushoto)
wakisoma taarifa fupi iliyoandaliwa na Mkuu wa Magereza wakati wa ziara ya Jaji
Mkuu mkoani Ruvuma.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akitambulishwa kwa viongozi wa Gereza la Mahabusu Songea wakati wa
ziara katika gereza hilo.
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania akitoka ndani ya gereza la mahabusu Songea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni