Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman (kushoto) Jaji Mfawidhi kanda ya Songea Mhe. John S. Mgetta (kulia) wakishiriki kukagua usahihi wa mwenendo wa Mashauri unavyorekodiwa kwenye Majalada lengo ikiwa kukagua utendaji kazi wa Mahakama kwa Wananchi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.
Mhe. Jaji Mkuu akipata maelezo ya Wilaya ya Mbinga kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mhe. Senyi Ngaga
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Katarina Revocatti, akipitia jalada moja baada ya jingine kuona hali halisi ya utoaji haki kwa Wananchi katika Mahakama ya Mwanzo Kigonsera mkoani Songea.
Jaji Mkuu Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akipokewa na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mbambabay Wilaya ya Nyasa wakati wa ziara kanda ya Songea.
Jengo la Mahakama ya Mwanzo Mbambabay Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni