Jumamosi, 19 Machi 2016

MKUTANO MKUU WA MWAKA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO MAHAKAMA.



Mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mahakama SACCOS Bibi Wanyenda P. Kutta Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Mahakama ya Tanzania akitoa risala fupi juu ya umuhimu wa watumishi kujiunga na kuendeleza vyama kwa ajili ya maendeleo yao binafsi na kuchangia katika uchumi wa taifa.



Mwenyekiti wa Chama cha ushirika wa akiba na mikopo Mahakama ya Tanzania, Bwana Iddi Mokiwa, akitoa taarifa fupi ya muelekeo wa chama mbele ya mgeni rasmi na wanachama wa Mahakama SACCOS, katika mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika Mahakama Kuu Dar es salaam.



Bwana Peter Christopher, Afisa Huduma za biashara benki ya CRDB (aliyesimama), akiwaelimisha wanachama wa Mahakama SACCOS juu ya Fahari Huduma inayotolewa na Benki ya CRDB,ambayo ni faida kwa wanachama wa vikundi ambayo huweza kutoa mikopo mikubwa na midogo ili kuweza kuwanufaisha wanachama.



Wanachama Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Mwaka, Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Mahakama, wakisoma na kufatilia agenda zilizowasilishwa katika mkutano, ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.





Mwanachama mwakilishi wa mkoa wa Mwanza (aliyesimama), akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo Mahakama.



Afisa Ushirika wa Wilaya ya Ilala (aliyesimama), akizungumzia lengo na dhumuni la kuwa na SACCOS ambayo itawasaidia kuinua wanachama kiuchumi na kijamii, katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni