Jumatatu, 21 Machi 2016

SEMINA YA MAFUNZO IDARA YA TEHAMA MAHAKAMA YA TANZANIA.

Bw. Machumu Essaba,Mkurugenzi  Msaidizi Idara Tehama Mahakama ya Tanzania(aliyesimama), akitoa maneno mafupi ya kumkaribisha Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Edward Nkembo katika mafunzo ambayo lengo kuu la Idara ni kuonesha na kuboresha mikakati ya utendaji kazi kwa ufanisi kwa watumishi wote wa Idara ya Tehama kwa Mahakama ya Tanzania.

Bw. Edward Nkembo,Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Mahakama ya Tanzania(aliyesimama), akitoa hotuba fupi ya kuelezea yale yanayohitajika  kwenye utawala wa Mahakama kutoka kwenye  Idara ya Tehama.  

Bw. Allan Machella, Afisa Tehama (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Semina ya Tehama kwa watumishi Mahakama ya Tanzania.
 Watumishi  washiriki wa Idara ya Tehama Mahakama ya Tanzania waliohudhuria mafunzo, katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

Bw. Edward Nkembo,Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Mahakama ya Tanzania(wa pili kushoto), Bw. Machumu Essaba,Mkurugenzi  Msaidizi Idara ya Tehama (wa pili kulia), Bw. Sebastian Lacha, Mkurugenzi Msaidizi Ufatiliaji na Tathmini (wa kwanza kushoto), Bw. Bakari Yusuph, Mshauri wa mambo ya Tehama (wa kwanza kulia), katika picha ya pamoja na Maafisa Tehama wa Mahakama  ya Tanzania, walioshiriki semina ya mafunzo.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni