Jumatano, 23 Machi 2016

SEMINA ELEKEZI KWA KURUGENZI YA TEHAMA MAHAKAMA YA TANZANIA -(IJA) LUSHOTO.


Bw. Bakari Yusuf Mtaalamu Mshauri wa mifumo ya kielektroniki wa Mahakama ya Tanzania akitoa mada juu ya mfumo wa kuratibu mashauri kwa maafisa TEHAMA wa Mahakama ya Tanzania. Katika mafunzo ya wiki moja yanayoendelea Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA)Lushoto.



Bw. Fredhope Gondwe Afisa TEHAMA na msimamizi wa Tovuti ya Mahakama (WEBMASTER) akitoa ufafanuzi kwa Maafisa TEHAMA jinsi tovuti hiyo pamoja na mifumo mingine inayolenga kuwashirikisha Wadau wa Mahakama katika kupata taarifa na kutoa maoni yao.

Bw. Allan Machella Afisa TEHAMA wa Mahakama ya Rufaa akitoa mada kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati (2015/2016 - 2019/2020) kwa Maafisa TEHAMA katika Semina ya Maafisa hao inayoendelea – Chuo Cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto.


Bw. Sebastian Lacha Mkurugenzi Msaidizi Mipango na Ufuatiliaji akitoa mada ya mpango mkakati wa Mahakama ya Tanzania.


Baadhi ya Maafisa TEHAMA walio hudhuria Semina katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni