Jumanne, 19 Aprili 2016

MHE. JAJI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA KANDA YA MBEYA.





  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akikaribishwa na Watumishi katika Mahakama ya Wilaya Mbozi mkoani Mbeya wakati wa ziara katika kanda ya Mbeya.

  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.




Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Kanda ya Mbeya. 

Katika ziara yake Mhe. Jaji Mkuu aliambatana na Maafisa na Watendaji kadhaa wa Mahakama kutoka Makao makuu ili kujionea hali ya utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kubainisha na kufanyia kazi changamoto ambazo watumishi wanakumbana nazo katika utendaji kazi wa kila siku. 

Ziara ya Mhe. Jaji Mkuu katika kanda hii imelenga kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika kanda hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha Watumishi wa Mahakama kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. 



Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Bw. Ahmad Namohe (aliyesimama), akimkaribisha rasmi Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya Mbozi, katika ziara ya kukagua hali ya utoaji Haki katika Mkoa wa Mbeya.

  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, akipata taarifa fupi ya Mahakama ya Wilaya Mbozi kutoka kwa Mhe. Asha H. Waziri, Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Mbozi, Kanda ya Mbeya (aliyesimama), mara baada ya kuwasili Mahakamani hapo.

 Mhe. Noel. P. Chocha Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya(kushoto), akimuonesha mazingira ya Mahakama ya Wilaya Mbozi Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, Msajili na viongozi mbalimbali waliombatana pamoja wakati wa ziara wilayani Mbozi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Bi. Edna Mwaigomole (katikati), akitoa maelezo machache kwa Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, Watendaji, Wasajili na Watumishi kuhusu eneo lililopatikana kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama Wilaya ya Mbozi.

  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania akikaribishwa Wakuu wa Usalama Mkoa wa Songwe, Watumishi katika Mahakama ya Wilaya Momba mkoani Songwe mara baada ya kuwasili wakati wa ziara ya kikazi katika wilaya ya Momba.

 Mkuu wa Wilaya ya Momba Bw. Richard Mbeho (aliyesimama), akimkaribisha Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (wa pili kushoto), Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (wa pili kulia), Mhe. Katarina Revocati, Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania (kulia) mara baada ya kuwasili katika Mahakama ya Wilaya Momba.

 Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya (kulia), akionyesha Jaji Mkuu wa Tanzania mazingira ya Ukumbi wa kusililiza kesi katika Mahakama ya Wilaya Momba.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni