Jumatano, 20 Aprili 2016

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA









                                                                 TAARIFA KWA UMMA

1.0 Katika gazeti la Mwananchi katika safu ya maoni ya Wananchi iliandikwa lalamiko lenye kichwa cha Habari ‘’ Kuna jipu Mahakama ya Wilaya ya Masasi ‘’ na Bw. Yohana Mbaga kutokana na kucheleweshwa kwa uamuzi wa Mirathi tangu 2009 katika Mahakama hiyo.


2.0 Ni kweli kuwa Mirathi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi na Bw. Yahaya Mbaga cha kusikitisha ni kuwa, kwa muda mrefu Bw.Yohana Mbaga alikuwa hatokei Mahakamani kuhususina na mirathi hiyo.

3.0 Baada ya kuona kuwa, msimazi wa Mirathi hiyo yaani Bw Yohana Mbaga hatokei katika shauri hilo la Mirathi Hakimu wa Wilaya ya Masasi alitoa maamuzi yafuatayo:

1. Alitengua usimamzi wa Mirathi hiyo na Bw.Yohana Mbaga.

2. Hakimu wa Wilaya aliamuru warithi wote wa Mirathi hiyo wakae kikao na kumchagua msimazi mwingine.

3. Nyaraka (original documents) Cheti cha kifo,stakabadhi ya cheti cha kifo alizoizacha msimazi wa mirathiakabidhiwe Bw.Yohana Mbaga.

4.0 Mahakama iko katika maboresho ya huduma zake ikiwemo maboresho katika mfumo mzima wa huduma za Mirathi kuanzia taratibu za ufunguzi wa Mirathi pamoja na malipo. Ili kuboresha huduma zetu, katika muundo wa Mahakama kumeundwa Kurugenzi ya Malalamiko na Maadili kushughulikia malalamiko mbalimbali kama hili la Bwana Yohana Mbaga. Hata hivyo, ili kuboresha zaidi huduma zetu Mahakama ya Tanzania hutumia namba ya simu 0754500400 au 0784821170. Namba hizi zinaweza kutumika na Mwananchi yeyote kutuma lalamiko au maoni kwa njia ujumbe mfupi waSMS au Whatsup ya namna bora ya kuboresha huduma za Mahakama ya Tanzania.

Mwisho tunapenda kuwashauri wadau wetu hasa wenye Mashauri ya Mirathi ni vyema kabala ya kufungua shauri la Mirathi Mahakamani wawe wamejipanga mapema nani atakuwa masimami wa Mirathi husika ili kupunguza malalamiko na ucheleweshwaji usio wa lazima kama ilivyotoke katika Mirathi hii Wilayani Masasi.

Imetolewa na:


Kitengo Cha Habari,Elimu na Mawasiliano

MAHAKAMA YA TANZANIA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni