Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu
wa Tanzania (kushoto), akisikiliza taarifa fupi ya Mkoa wa Mbeya kutoka kwa
Mhe. Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa huyo wakati wa
ziara mkoani humo.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu
wa Tanzania (wa pili kulia) akipata taarifa fupi ya utendaji kazi wa Mahakama
Kanda ya Mbeya kutoka kwa Mhe. Noel. P. Chocha, Jaji Mfawidhi Kanda ya Mbeya
(aliyesimama), mara baada ya kuwasili katika kikao kilichohusisha Mahakimu
Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya
Mbeya.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu
wa Tanzania akizungumza na Mahakimu
Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya
Mbeya alipokutana nao na kuwaasa kuendelea kutenda Haki kwa wakati ili kuweza
kupunguza na kumaliza mashauri yanayowasilishwa mahakamani.
Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu wa
Mahakama ya Tanzania (aliyesimama) akizungumza na Mahakimu Wakazi
Wafawidhi,Watendaji, Maafisa Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya wakati
wa ziara.
Bi. Agripina Mwamanda, Mkutubi wa Maktaba
ya Mahakama Kuu Mbeya (aliyesimama),
akichangia mada na kuuliza maswali kwa Jaji Mkuu wakati wa kikao kifupi kilichoandaliwa kuhusu
utendaji kazi wa Mahakama kwa Kanda ya Mbeya.
Naibu Msajili,Mahakimu Wakazi Wafawidhi,Watendaji, Maafisa
Utumishi na Maafisa Tawala wa Kanda ya Mbeya waliokutana na kuzungumza na Jaji Mkuu wa Tanzania kuhusu utendaji kazi Mahakama kwa Kanda ya Mbeya.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa
Tanzania akioneshwa ramani ya jengo la Mahakama Kuu Mbeya ambalo lipo kwenye ukarabati.
Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu
wa Tanzania (wa pili kushoto), Jaji Mfawidhi kanda ya Mbeya(kulia),Mhe. Hussein Kattanga Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wakikagua ukarabati unaoendelea
katika jengo la Mahakama Kuu Mbeya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni