JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAHAKAMA
TANGAZO
YAH:
WASHINDI WA SHINDANO LA KUSANIFU BENDERA NA NEMBO YA MAHAKAMA
1.
Kwa mujibu wa Katiba kifungu 107 (A) Mamlaka ya utoaji haki katika
Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama. Sheria ya Bendera na Nembo ya Taifa,
sura ya 10 kifungu cha 6 (1) inaruhusu taasisi yoyote ya Serikali ama Umma kuwa
na Bendera yake ambayo ndani yake itakuwa na Bendera ya Taifa, Nembo ama alama
yoyote ilivyooneshwa katika kifungu 6 (1) cha sheria ya bendera na Nembo ya
Taifa.
2.
Mahakama ya Tanzania,
ilitoa tangazo tarehe 29 Aprili 2015 katika magazeti ya Daily News,Mwananchi
pamoja na The Gurdian kuhusu shindano la kusanifu Nembo na Bendera ya Mahakama.
Jumla ya washiriki 224 walituma michoro yao. Baaada ya kupitia kwa kina na
kamati maalumu ya wataalamu, wafauatao wanataarifiwa kuwa wameteuliwa kuwa washindi
wa shindano hilo kama ifutavyo:
i)
Clarance J.Mhoja
ii)
Emanuel Makene/Patric
Mwakitosi
iii)
Charles Kitanda
iv)
Moses Luhanga
v)
Huruma S.Mpombo
vi)
Lightness Sirikwa
vii)
Zena Kidabu
viii)
Mwidadi M.Msangi
ix)
Jeremiya Mayeye
x)
Hamisi Salum Fundi
3.
Washindi tajwa hapo
juu wanaomba kuwasiliana na Ofisi ya Mtendaji Mkuu Mahakama, iliyopo barabara ya kivukoni nyumba
namba 26 ili kupata taratibu kutunukiwa zawadi zao. Barua za maelekezo
zimetumwa kupitia anuani zenu.
4.
Mahakama ya Tanzania
inawashukuru wote waliotuma michoro yao na tunathamini michango yenu yote.
Imetolewa na:
MTENDAJI MKUU,
MAHAKAMA YA TANZANIA,
26 BARABARA YA KIVUKONI,
S.L.P 9004,
11409 DAR ES SALAAM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni