Ijumaa, 27 Mei 2016

MAAFISA TAWALA KANDA YA IRINGA WASISITIZWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU.


Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa Bw. Elvin H. Mwakajinga(pichani), amewasisitiza Maafisa Tawala wa Wilaya wote wa Kanda ya Iringa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu makarani wao katika zoezi la uingizaji wa kesi zote kwenye mfumo wa "JSDS". Lengo ikiwa ni kuhakikisha Mahakama Kuu Kanda ya Iringa inaendelea kuwa imara katika uboreshaji wa huduma zitolewazo na Mahakama katika utumiaji wa Mfumo wa Dashboard na mifumo mingine yote itakayokuwa inaanzishwa na Mahakama ya Tanzania.
 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Iringa Mhe. Isaya (kulia) pamoja na Maafisa Tawala na Watumishi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa wakimsikiliza Mtendaji wa Mahakama Iringa.
Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Iringa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni