Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza Mhe. Robert Makaramba (aliyesimama) akisoma hotuba kwa niabaya Mhe.
Mohamed Chande Othman Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Robert
Makaramba amemuwakilisha Jaji Mkuu katika kongamano la siku ya Uhuru wa Habari
Duniani katika ukumbi wa Malaika Beach Resort Jijini Mwaza.
Akisoma hotuba, kwa
niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Mohamed Chande Othman alisema kuwa, ni
nia ya Mahakama kuona kuwa Uhuru wa
kupata habari na vyombo vya habari unapewa kipaumbele kwa mujibu wa sheria na
kanuni zilizopo. Mhe.Jaji Mkuu alisema
kuwa vyombo vya Habari ni nguzo muhimu sana katika kupambana na ukiukwaji wa
haki za binadamu. “Katika jamii yoyote ya kidemokrasia,vyombo huru vya habari
ni silaha muhimu sana katika kurahasisha utawala bora na maendeleo” alisema Jaji
Mkuu.
Mhe.Jaji Mkuu
alisema kuwa, kwa kutambua changamoto za upatikanaji na utoaji wa taarifa,kote
kwa watumishi wa Mahakama na waandishi
wa habari, Mahakama imechukuwa hatua kadha kuleta mahusiano mema na vyombo vya habari.
Mahakama kwa kushirikiana na Baraza la Habari
Tanzania (MCT) yalianzishwa mafunzo maalum kwa waandishi habari
wanaondikia Mahakama yakilenga namna
bora ya kuripoti habari za Mahakama na matunda yake tumeanza kuyaona kwa kufuatilia
habari mbalimbali katika vyombo vya Habari.
Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA) imeanzisha mafunzo maalum yahusuyo upatikaji na utoaji wa taarifa na huduma kwa wateja kwa watumishi wa kada mbalimbali za Mahakama. “Mtaona kuwa kwa uhakika juhudi hizo kwa kiasi kikubwa inaendana na dhima ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari nchini ‘’ alisisitiza Jaji Mkuu.
Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA) imeanzisha mafunzo maalum yahusuyo upatikaji na utoaji wa taarifa na huduma kwa wateja kwa watumishi wa kada mbalimbali za Mahakama. “Mtaona kuwa kwa uhakika juhudi hizo kwa kiasi kikubwa inaendana na dhima ya siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari nchini ‘’ alisisitiza Jaji Mkuu.
Mhe. Jaji Mkuu
alitoa changamoto zilijitokeza wakati wa kuripoti uchaguzi mkuu kwa mwaka 2015 kwa baadhi ya vyombo vya Habari kuegemea na
kuonesha mapenzi binafsi na vyama au wagombea Fulani. “Ni
tabia ya baadhi ya vyombo vya habari kutumia matusi,kashfa na maneno ya kejeli
ni ya kawaida kwenye jamii, ambayo viwango vya weledi vinazingatia ukweli,usawa
na kuwajibika havijahafikiwa” alifafanua Jaji Mkuu.
Mhe.Jaji Mkuu
alimalizia kwa kusema kuwa Mahakama inaamini haki za msingi za kujieleza,kujihusisha
na uhuru wa vyombo vya habari, na haki ya kupata taarifa kama katiba
invyosema.Mahakama inaamini kuwa uwepo wa sheria nzuri za vyombo vya habari na upatikaji wa taarifa ni chachu kubwa ya
maendeleo katika nchi.
Wanahabari na
Wadau wa Habari wakiwa katika katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2016 yanayofanyika Kitaifa katika Hotel ya
Malaika Beach Resort Jijini Mwanza.
Bw. Reginald Mengi, Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (aliyesimama), akisoma risala fupi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani kwa 2016.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza Mhe. Robert
Makaramba (wa nne toka kulia),pamoja na meza kuu walioketi, katika picha ya pamoja Wanahabari na
Wadau wa Habari wakiwa katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa
Vyombo vya Habari Duniani 2016,yaliyofanyika mkoani Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni