Ijumaa, 6 Mei 2016

JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA AFUNGUA MAFUNZO YA HUDUMA KWA WATEJA KWA WATUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI MWANZA.

Mhe. Robert V.Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,  akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe.Robert Vicent Makaramba, amewataka watumishi wa Mahakama Mkoani Mwanza kutimiza wajibu wao kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na kwa wakati.

Mhe.Makaramba ameyasema hayo hii leo Jijini Mwanza, wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.

Amesema Mafunzo hayo yamekuja kwa wakati ikizingatiwa kwamba Mahakama ya Tanzania kwa sasa inaendelea na maboresho ya Utendaji kazi wake kama sehemu ya kuhakikisha kwamba inatoa huduma iliyo bora kwa wananchi.

Mwenyekiti wa taasisi ya MISA tawi la Tanzania, Simon Berege, amesema mafunzo hayo yanaendeshwa katika Kanda zote za Mahakama nchini, baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2014 kuonyesha kwamba kuna ugumu katika upatikanaji wa habari za mahakama kwa umma hata kama habari hizo siyo za siri.

“Tunaipongeza Mahakama kwa hatua hii ya kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wake na kutoa taarifa muhimu kwa wananchi maana mihimili mingine imekuwa ikiminya upatikanaji wa taarifa zake hata kama taarifa hizo siyo za siri”. Amesema Berege.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema wanatarajia kujifunza mambo mengi ikiwemo kuongeza ujuzi zaidi wa namna ya kuwahudumia wateja (Wananchi) ili kuwafanya watambue kwamba Mahakama nchini zinatenda haki.


Mafunzo hayo ambayo yanafadhiriwa na Shirika la Misaada la Ujerumani FES, yamefanyika Mkoani Mwanza baada ya mafunzo kama hayo yaliyofanyika katika Mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tabora kuonyesha yameongeza ufanisi na utendaji wa Watumishi wa Mahakama katika kuwahudumia wananchi hususani katika utoaji wa taarifa kwa umma ambapo yanawajumuisha Mahakimu,Maafisa Tawala,Watunza Kumbukumbu, Makatibu Mahsusi pamoja na Maafisa Utumishi wa Mahakama.
Washiriki wa Mafunzo ya Huduma kwa Wateja wakimsikiliza Mhe.Robert Vicent Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,(aliyesimama) katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mhe.Robert Vicent Makaramba, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza,  akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MISA-TANZANIA, Simon Berege, akizungumza katika Ufunguzi wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.

Bw.Gasirigwa Sengiyumva, Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, akizungumza katika Mafunzo hayo.
Afisa Habari na Utafiti kutoka MISA-Tanzania, Gasirigwa Sengiyumvya, akizungumza katika Mafunzo hayo
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama mkoani Mwanza.

Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza
Washiriki wa Mafunzo Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama mkoani Mwanza.
Mgeni Rasmi, Mhe.Robert Vicent Makaramba Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoa wa Mwanza.
Mgeni Rasmi, Mhe.Robert Vicent Makaramba, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Maalumu ya huduma kwa Wateja yanayotolewa kwa Watumishi wa Mahakama za Mkoani Mwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni