JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME
YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
TANGAZO
LA NAFASI 58 ZA KAZI.
1.0 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo
kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa
Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama
Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine
inalo jukumu la kuajiri watumishi wa
kada mbalimbali wa Mahakama.
1.1
Hivyo,
Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa
hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi kwenye
kituo chochote Tanzania Bara, katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko
katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II, Mhasibu Daraja
la II, Mhasibu Msaidizi, Afisa Utumishi Daraja la II, Afisa Tawala Daraja la
II, Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Daraja la
II, Afisa Ugavi Daraja la II, Katibu Mahsusi Daraja la III, Msaidizi wa
Kumbukumbu Daraja la II, Msaidizi wa Maktaba, Mpokezi , Msaidizi wa Ofisi na Mlinzi.
1.2
Tafadhali
soma kwa makini na kuzingatia maelekezo yote yaliyoorodheshwa katika sehemu ya
kumi na sita ya tangazo hili.
2.0 Hakimu
Mkazi Daraja la II – TJS 2 - Nafasi
- 20
2.1 Sifa:-
·
Waombaji wawe
na shahada ya kwanza ya Sheria “Bachelor
of Laws” (LLB) kutoka katika Chuo kikuu kunachotambulika na Serikali pamoja
na cheti cha mafunzo ya Sheria kwa
vitendo (Law school Certificate).
2.2 Kazi za kufanya:-
(i)
Kuandaa
mpango wa kusikiliza mashauri.
(ii) Kusikiliza mashauri
ya awali ya Jinai(Criminal Cases), Madai (Civil Cases), Mirathi (Probate
and Administration) na ndoa (Matrimonial Cases).
(iii)
Kutoa
hukumu katika mashauri yote
anayoyasikiliza ya jinai, madai,
mirathi, ndoa na mashauri mengine, kadri
sheria inavyomruhusu.
(iv)
Kutoa
amri mbalimbali za kimahakama anazoruhusiwa kisheria katika Mahakama za Mwanzo.
(v) Kusuluhisha mashauri.
(vi)
Kusikiliza
rufani kutoka Mabaraza ya Kata.
3.0. Afisa Utumishi Daraja la
II (TGS D) - Nafasi - 3.
3.1 Sifa:-
Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Jamii
au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali
ambao wamejiimarisha (major) katika
mojawapo ya fani zifuatazo:-
·
Menejimenti
ya RasilimaliWatu (Human Resource Management)
·
Elimu
ya Jamii (Sociology)
·
Utawala na Uongozi (Public Administration)
·
Mipango
ya Watumishi (Manpower Planning)
·
Wawe
na ujuzi wa kutumia kompyuta.
·
3.2 Kazi
za Afisa Utumishi Daraja la II:-
(i)
Kutunza
Kumbukumbu sahihi za watumishi
wote
(ii) Kutafsiri na kushughulikia
utekelezaji wa miundo ya utumishi.
(iii) Kutafiti, kuchanganua,
kupanga na kukadiria idadi ya watumishi
wanaohitaji mafunzo.
(iv) Kukusanya, kuchambua na
kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi.
(v) Kushughulikia masuala
mbalimbali ya kila siku ya watumishi
(vi) Kusimamia OPRAS.
4.0 Afisa
Tawala Daraja la II – TGS D – Nafasi - 1
4.1 Sifa:-
Shahada ya kwanza
kutoka vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo:-
Utawala, Elimu ya Jamii, Menejimenti ya Umma, Uchumi na
wenye ujuzi wa kompyuta
4.2
Kazi
za Maafisa Tawala:-
(i)
Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu
(ii)
Kusimamia
utekelzaji wa Sheria, Sera, Kanuni na taratibu
mbalimbali
(iii)
Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji
5.0 Afisa Ugavi Daraja la II
– TGS D – Nafasi – 2
5.1 Sifa:-
Shahada ya Biashara (B.Com) yenye mchepuo wa ugavi au
Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management)
inayotolewa na vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamaizi wa
Vifaa.
5.2
Kazi
za Maafisa Ugavi:-
(i) Kukusanya
takwimu za kuweza kusaidia kutayarisha makisio ya vifaa vinavyohitajika.
(ii)
Kuandaa
mpango wa manunuzi.
(iii) Kukusanya
na utunzaji wa takwimu za utendaji za wazabuni mbalimbali.
(iv) Kukusanya
na utunzaji wa takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
(v)
Kusimamia
utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
(vi) Kusimamia
upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa.
(vii)
Kusimamia
ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara.
6.0 Mkaguzi
wa Hesabu wa Ndani Daraja la II (Internal Auditor Grade II) TGS D - Nafasi 1
6.1 Sifa
(i) Wenye ‘Intermediate Certificate’
inayotolewa na NBAA
(ii) Wenye
Shahada ya Biashara au Sanaa yenye mwelekeo wa Uhasibu
au Stashahada ya juu ya Uhasibu (ADA) kutoka Chuo/Taasisi
yoyote inayotambuliwa na serikali.
(iii) Wenye
stashahada ya juu katika Uhasibu wa Serikali
(Advanced Diploma in Government
Accounting) kutoka chuo
cha Uhasibu Dar es salaam (DSA).
6.2 Kazi za
Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Daraja la II
(i)
Kufanya
Ukaguzi wa hesabu
(ii)
Kusahihisha
na kuidhinisha ripoti ya Ukaguzi
(iii)
Kusahihisha
na kuidhinisha hoja za ukaguzi wa ndani
(Internal
Audit queries)
7.0 Mhasibu Daraja
la II TGS D – Nafasi 6
7.1 Sifa:-
(i) ‘Intermediate Certificate’ inayotolewa na
NBAA.
(ii) Shahada ya Biashara/Sanaa yenye mwelekeo wa
uhasibu au Stashahada ya juu ya Uhasibu kutoka Chuo Kikuu/ Taasisi yoyote
inayotambuliwa na Serikali.
(iii) Stashada ya Juu ya Uhasibu Serikalini
(Advanced Diploma in Government Accounting) inayotolewa na Chuo cha Uhasibu
kinachotambuliwa na Serikali.
7.2 Kazi
za kufanya:-
(i) Kuidhinisha hati za malipo.
(ii) Kuandika taarifa ya mapato na matumizi ya
mwezi.
(iii) Kusimamia Wahasibu Wasaidizi katika kazi
zao za kila siku.
(iv) Kusimamia shughuli za uhasibu kwenye
Kitengo cha Idara.
(v) Kuandika taarifa ya maduhuli.
8.0 Mhasibu
Msaidizi TGS C - Nafasi 3
8.1 Sifa
(i)
Kuajiriwa wenye cheti cha ufaulu mtihani mgumu
wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy Examination)
unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma au
(ii)
Wenye Stashahada ya Kawaida ya Uhasibu kutoka
Chuo/Taasisi yoyote inayotambiliwa na Serikali. Aidha mwenye uzoefu usiopungua
mwaka mmoja (1) katika fani hiyo atafikiriwa kwanza.
8.2
Kazi za kufanya:-
(i)
Kupokea
na kulipa fedha
(ii)
Kutunza
daftari la fedha
(iii)
Kufanya
usuluhisho wa hesabu za benki
(iv)
Kukagua
hati za malipo
(v)
Kupitisha
malipo kulingana na kanuni za fedha
(vi)
Kusimamia
kazi za Wasaidizi wa Hesabu.
9.0 Katibu
Mahsusi Daraja la III TGS B – Nafasi 2
9.1
Sifa:-
Kuajiriwa wahitimu
wa kidato cha IV
waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
mtihani wa Uhazili Hatua ya
Tatu.
Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (Shorthand) maneno 80 kwa dakika moja
na wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu
za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
9.2
Kazi
za kufanya:-
Katibu Mahsusi Daraja la III atapangiwa kufanya kazi Typing pool au chini
ya Katibu Mahsusi mwingine
mwenye cheo cha juu kumzidi
kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu au
kitengo.
(i)
Kuchapa
barua, taarifa na nyaraka za kawaida
(ii)
Kusaidia
kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanazoweza
kushughulikiwa.
(iii)
Kusaidia kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao
safari za Mkuu wake na
ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi
anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu
wake kwa wakati unaohitajika.
10 .0 Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la
II TGS B – Nafasi 7
10. 1 Sifa
za Kuingilia:-
Kuajiriwa wahitimu wa
kidato cha nne au sita wenye cheti/Stashahada ya utunzaji kumbukumbu katika
mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.
10.2
Kazi za kufanya:
(i) Kutafuta
kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji.
(ii) Kudhibiti upokeaji,
uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
(iii) Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki
(file racks/cabinets) katika masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
(iv) Kufanya kazi nyingine
za kiutawala zinazohusu masuala ya kimahakama kama kuwasilisha nyaraka za
kisheria Mahakamani na kuangalia muda na siku ya kufanyika kwa kesi husika.
(v)
Kufanya kazi nyingine
atakayopangiwa.
11 Msaidizi
wa Maktaba Daraja la II TGS B - Nafasi 1
11.1 Sifa
za Kuingilia:-
Kuajiriwa wenye cheti cha Mtihani wa kitaifa
wa kidato cha IV ambao wamefaulu mafunzo
ya Wasaidizi wa Maktaba (National Library Assistants Certificate Course)
yatolewayo na Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania au wenye cheti kinacholingana
na hicho.
11.2 Kazi
za kufanya:-
(i)
Kuandikisha
wasomaji
(ii)
Kupanga
vitabu katika rafu (Shelves)
(iii)
Kuazimisha
na kupokea vitabu vinavyoazimwa
(iv)
Kukarabati
vitabu vilivyochakaa
(v)
Kazi
nyingine atakazopangiwa na mkuu wa kituo.
12.
0 Mpokezi TGS A – Nafasi – 1
12.1 Sifa:-
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na
Hisabati na Kufuzu mafunzo ya mapokezi na upokeaji simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
12.2 Kazi
za kufanya:-
(i)
Kupokea
wageni na kuwasilisha shida zao
(ii)
Kutunza
na kudumisha usafi wa “ Switchboard” na Ofisi yake,
(iii)
Kupokea
simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maafisa mbalimbali Ofisini.
(iv)
Kupokea
simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi,
(v)
Kutunza
rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa nje ya ofisi.
13.0 Msaidizi wa Ofisi TGOS A – Nafasi - 5
13.1 Sifa:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliofaulu vizuri katika masomo ya
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
13.2 Kazi za
kufanya:-
i.
Kufanya
usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta
vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia
bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua na miti na kusafisha vyoo.
ii. Kuchukua
na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofisa wanaohusika na kuyarudisha
sehemu zinazohusika.
iii.
Kusambaza
barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
iv.
Kutayarisha
chai ya ofisi
v.
Kupeleka
mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka
Posta.
vi.
Kuhakikisha
kwamba vifaa vya ofisi vinawekwa sehemu zinazostahili.
vii.
Kufunga
Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa
asubuhi na Jioni na kuyafunga baada ya saa za kazi.
viii.
Kudurufu
barua au machapisho.
ix.
Kuweka
katika majalada nakala za barua zilizochapwa
katika ofisi walizomo.
x.
Kutunza
vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
14.0 Mlinzi TGOS A – Nafasi - 6
14.1 Sifa:-
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne
waliofuzu mafunzo ya Mgambo/Polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika
chuo kinachotambuliwa na Serikali.
14.2 Kazi za
kufanya:-
(i)
Kuhakikisha
kwamba mali yote inayotolewa mlangoni
(nje ya ofisi) ina hati ya
idhini.
(ii) Kuhakikisha kwamba mali yote inayoingizwa langoni inazo
hati za uhalali wake.
(iii) Kulinda usalama wa majengo, ofisi na
mali za ofisi mchana na usiku.
(iv) Kuhakikisha kwamba milango na
madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho
wa saa za kazi.
(v) Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la
ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
Mwisho wa kupokea barua za maombi
hayo ni tarehe 15/06/2016 saa 9:30
Alasiri.
15.0 Barua za maombi
ziandikwe kwa mkono wa mwombaji na kuambatisha:-
-
Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo.
-
Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV).
-
Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
-
Picha mbili (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni.
16.0 Aidha,
inasisitizwa kwamba:-
16.1 Waombaji wawe
na umri kati ya miaka kati ya 18 na 44
16.2 Waombaji wa kazi toka maeneo husika na wenye
sifa zilizoainishwa katika tangazo hili, watafikiriwa kwanza na kupangiwa kazi
katika maeneo husika.
16.3 Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji.
16.4 Waombaji walio katika Utumishi wa Umma
wapitishe maombi yao kwa waajiri wao wa
sasa.
16.5 Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa
Umma waeleze kwamba waliacha kazi
Serikalini na sababu ya kufanya hivyo.
16.6 Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa
watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania.
16.7 Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao
vithibitishwe na TCU/NACTE wakishindwa kutekeleza hili maombi yao
hayatashughulikiwa.
16.8 Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa
kirefu.
16.9 Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba
nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao.
16.10 Waombaji waliowahi kufukuzwa kazi wasiombe.
16.11 Waombaji wasio na sifa zilizotajwa na ambao
hawatazingatia masharti yaliyotajwa hapo
juu maombi yao hayatashughulikiwa.
16.12 Waombaji watakaotoa taarifa za uongo mfano
kuhusu umri wao, elimu yao au sehemu
walizowahi kufanyia kazi na ikagundulika hata kama watakuwa wameshaajiriwa watachukuliwa
hatua kali za kisheria.
17.0 Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM.
Imetolewa na ;-
Katibu,
Tume ya Utumishi wa Mahakama,
S.L.P
8391,
DAR
ES SALAAM,
TANZANIA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni